LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2021

MFUKO WA WCF WASHUSHA VIWANGO VYA UCHANGIAJI KUTOKA ASILIMIA 1 HADI ASILIMIA 0.6.

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeshusha viwango vya uchangiaji kwenye Mfuko huo kutoka asilimia 1 hadi asilimia 0.6 ambayo sasa Waajiri kutoka Sekta Binafsi watachangia kutoka mishahara ya wafanyakazi wao.


CWF imepunguza hadi kufikia kiwango hicho cha asilimia 0.6 kutokana na uamuzi wa Serikali.


Akitangaza punguzo hilo kwa waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salam leo Julai 26, 2021, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk. John Mduma amesema waajiri wote kutoka sekta binafsi wataanza kuchangia kiwango hicho kipya cha asilimia 0.6 ya mshahara wa mfanyakazi kuanzia mwezi huu wa Julai, 2021.


Amesema lengo la mabadiliko hayo ya kiwango cha uchangiaji ni kumpunguzia mzigo mwajiri ili fedha alizokuwa akitumia kuchangia azielekekeze kwenye maeneo mengine ya uendeshaji wa shughuli zake za uzalishaji.


“ Uamuzi huu ni utekelezaji wa maelekezo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani,amekuwa akitoa kuhusu Taasisi za Serikali kuhakikisha zinaweka mazingira bora ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini ili kukuza uchumi wa Nchi na kulinda Rasilimali Watu” Alisema.


Aliwahakikishia waajiri na waajiriwa kuwa licha ya punguzo hilo, Mafao yanayotolewa na Mfuko yatabaki kama yalivyokuwa kama ambavyo sheria iliyoanzisha Mfuko huo ya mwaka 2016 inavyoelekeza.


“ Tuliona hili liwekwe bayana isije kuonekana kwamba kwa kupunguza kiwango cha uchangiaji basi huenda na Mafao nayo yatapungua, la hasha Mafao yatabaki kama yalivyo kwani tumejihakikishia kwa kushirikiana na wataalamu kuwa kwa kufanya hivyo Mfuko utabaki imara na kuwa endelevu.” Amesema Mkurugenzi huyo.


Aidha Dk. Mduma alisema mchakato huo umepitia sehemu mbalimbali na kutoa shukrani kwa Chama Cha Waajiri nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kwa kushirikiana na Mfuko kufikia katika jambo hio.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dk. John Mduma (katikati) akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji, Anselim Peter na kulia ni Dk. Abdulsalaam Omar, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dk. John Mduma, akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),  Laura Kunenge (aliyesimama), akiongoza mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wakisikiliza
©CCM Blog/2021

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages