LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 28, 2021

*SIKU 100 ZA RAIS SAMIA NAOMBA ZIRUDIWE, ZIRUDIWEE - SEHEMU III*

 

Na Emmanuel J. Shilatu

Siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano w
a Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan zimetimia kwa mafanikio tele. Leo tuendelee kutazama mafanikio zaidi ambayo sio ya mwisho kimaana bali yameonyesha tija ya kazi inaendelea.

26. Rais Samia amesimamia vyema utawala wa sheria kwa kuhakikisha anailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

27. Rais Samia ameendelea kuulinda na kuutetea Muungano ulioasisiwa mwaka 1964. Kwa mamlaka makubwa aliyonayo Rais angeweza kufanya lolote, lakini hakuweza kufanya na ameendelea kuilinda katiba aliyoapa kwa kuulinda na kuutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

28. Rais Samia ameendelea kuwaunganisha Watanzania wote pasipo kujali itikadi zao, makabila yao, rangi zao wala imani zao. Chini ya utawala wa Rais Samia Watanzania wameendelea kuwa wamoja.

29. Ndani ya siku 100 Rais Samia amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii kama vile Wazee, Wanawake, Vijana, Wafanyabiashara, Viongozi wa dini, Bunge na sekta binafsi. Huko kote amesikiliza kero, ametatua changamoto na kutoa dira yenye matumaini makubwa ya ukombozi.

30. Rais Samia ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama ameendelea kuimarisha ulinzi na usalama ambapo mpaka sasa Watanzania tumeendelea kuishi kwa amani na usalama nyakati zote.

31. Ndani ya siku 100 Rais Samia amesajili miradi 93 yenye thamani ya USDBilioni 1.6 ambayo itaingiza ajira zaidi ya 24,600 kwa Vijana.

32. Ndani ya siku 100 Rais Samia amefanikiwa kuondoa tozo vikwazo kwa Wafanyabiashara zaidi ya tozo 232. Kitendo cha Rais Samia kuondoa tozo hizo ili kuwawezesha Wafanyabiashara kufanya biashara zao hapa nchini. 

33. Rais Samia ameendelea kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Watu hapa nchini. Kwa Rais Samia ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya yenye amani, furaha na hoja zaidi.

34. Ndani ya siku 100 tumeshuhudia Serikali ya Rais Samia ikiongeza bajeti ya elimu ya juu. Maana yake Wanafunzi wengi watakopeshwa mikopo, Wanafunzi wengi watapata elimu ya juu. Hapa adui ujinga anapigwa nje ndani kivitendo.

35. Ndani ya siku 100 tumeshuhudia kesi za muda mrefu zikimalizwa na hatma ikijulikana kwa kufuata taratibu zote kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za nchi. Kesi nyingi kumalizwa kwa kusikilizwa kwa haraka jambo ambalo linaipunguzia mzigo Serikali kuwahudumia Watuhumiwa mahabusu na kutoa pumziko na faraja kwa waliokuwa wanasota mahabusu.

..... Itaendelea ....

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages