LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 29, 2021

MAJALIWA AZINDUA MPANGO WA TATU WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO 2021/2022 – 2025/2026JIJINI DODOMA

 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026, uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Hamadi Masauni,akizungumza katika uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026, uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba,akielezea wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026, uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Sekta Binafsi,Azaki Mbenna,akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026, uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Nchini Tanzania, Christine Musisi,akizungumza wakati wa  uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026, uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati akizindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026,uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha vitabu vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 baada ya kuzindua mpango huo, hafla iliyofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 baada ya kuzindua mpango huo,uliofanyika leo June 29,2021  jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 baada ya kuzindua mpango huo, uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Cpt. Mst. George Mkuchika kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 kwa niaba ya Mawaziri wengine, baada ya kuzindua mpango huo uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Mhandisi Zena Said  kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 baada ya kuzindua mpango huo, uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela  kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 baada ya kuzindua mpango huo,kwa niaba ya wakuu wa Mikoa yote Tanzania bara uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

      

Baadhi ya Washiriki wa Hafla ya  uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026 wakimsilikiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma. 

   

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022-2025/2026  uliofanyika leo June 29,2021 jijini Dodoma.

Picha na Alex Sonna na  Ofisi ya Waziri Mkuu

……………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI Mkuu ,Kassim Majaliwa amezindua mpango tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano,2021- 2022/ 2025-2026 ambapo amesema Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha malengo ya mpango huu yanatimia.

Akizungumza leo,June 29,2021,jijini Dodoma wakati wa uzinduzi huo Jijini Dodoma,Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha malengo ya mpango huu yanatimia.

“Kamwe hatuwafumbia macho wazembe,wabadhirifu na Wala rushwa,Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha malengo ya mpango huu yanatimia,”amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amevitaja vipaumbele katika mpango huo ni pamoja na kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji wa huduma,kukuza uwekezaji wa biashara.

Amevitaja vipaumbele vingine ni kuchochea uchumi shindani na shirikishi,kuchochea Maendeleo ya watu,kuendeleza rasilimali watu.

Amesema makadirio ya gharama za mpango huo ni shilingi trilioni 114.8 ambapo Serikali itatoa shilingi trilioni 74.2 na Sekta Binafsi shilingi trilioni 40.6.

Hata hivyo amesema bado kuna changamoto ya utofauti wa vipato kwa watu, upungufu wa ajira,mabadiliko ya Tabia nchi,Mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

“Napenda kuwahakikishia Serikali yenu imejipanga vyema kukabiliana na changamoto hizi,”amesema.

Pia,amesema mambo yote waliyoahidi katika uchaguzi wakati wa kipindi cha kampeni amesema watajitahidi kutatekeleza kupitia mpango huu.

Vilevile,ameitaka Wizara ya fedha kutoa elimu huku akiagiza ofisi zote ziwe na nakala za mpango huu.

Amesema tathmini itafanyika kila mwaka hivyo Wizara na Tasisi zinatakiwa kuangalia jinsi ya kuutekeleza.

Waziri Mkuu amesema Tathmini ya mpango uliopita umekuwa na mafanikio kutokana na utekelezaji wa mambo muhimu kwenye sekta ya elimu bila malipo,sekta ya umeme kusambaza maji mijini na vijijini pamoja na upatikanaji wa maji,afya,kilimo,Viwanda,masoko ya uhakika.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu Majaliwa amemshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Jakaya Kikwete kwa kumwona na kumchagua kwa mara ya kwanza kuwa Mkuu wa Wilaya.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kunitoa darasani na kunichagua kuwa Mkuu wa Wilaya na baadae kwenda Jimboni na kuniteua kuwa Naibu Waziri wa Elimu,”amesema.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, amesema miradi ya kielelezo itaendelea kutekelezwa ambayo ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (SGR),Kufufua umeme wa maji Julius Nyerere (JNHPP) MW 2,115,Kuboresha Shirika la Ndege (ATCL),ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania.

Amevitaja miradi mingine ni Kiwanda cha Sukari Mkulanzi,Ujenzi wa madaraja makubwa na madaraja ya juu,kufua umeme wa maji Ruhudji MW 358,Makaa ya Mawe Mchuchuma na Liganga.

Katibu huyo ameitaja miradi mingine ni ufufuaji wa mafuta na gesi katika kitalu cha Eyasi Wembere,Kusindika Gesi asilia Lindi,Ujenzi wa reli ya kusini,Kanda Maalum ya kiuchumi na maeneo Maalum ya uwekezaji,Mradi wa magadi,utafutaji wa mafuta na gesi wa Mnazi Bay na kuongeza rasilimali watu wenye ujuzi.

Amesema mpango wa tatu ni mwendelezo wa jitihada za Serikali kusimamia rasilimali za ndani ya Nchi ikijumuisha Madini,maliasili,gesi asili,ardhi,fedha na rasilimali watu kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya watanzania wote.

Kwa upande wake,Mwakilishi wa Sekta Binafsi,Azaki Mbenna amesema wakiutazama mpango huo ni dira na ni mpango kazi na kwa wale wanaopenda Soka ni kiwanja cha nyumbani.

“Tukianza na ushirikiswaji tumeshirikishwa tangu mwanzo,angalia vipaumbele vyote vitano ndiko sekta binafsi iliko,”amesema

Amesema wanaahidi zile fedha trilioni 40.6 itazitoa huku ikitaka Mazingira wezeshi katika ufanyaji wa biashara.

Naye,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Hamadi Masauni amesema mpango huo ni muhimu ambapo maandalizi ya mpango huo yameshirikisha wadau mbalimbali na ni jumuishi.

Amesema Serikali ineanza maandalizi ya dira mpya ambayo itaendeleza maono ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya watu.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages