LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 22, 2021

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM CHAFANYIKA CHINI YA MWENYEKITI WA CCM, RAIS SAMIA, JIJINI DODOMA, LEO

CCM Blog, Dodoma, leo.

Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefanyika leo jijini Dodoma, kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.


Kikao hicho ambacho ni cha kawaida na cha kwanza kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, kimefanyika kujadili masuala mbalimbali ya Chama.


Kikao hicho kimefanyika baada ya Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika jana Juni 21, chini ya Mwenyekiti wake, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Picha👇

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan, akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kuingia kwenye Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika leo Jumanne Juni 22, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla akiongozana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, kwenda Ukumbini kwenye Kikao cha Kamati Kuu (Cc) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika leo Jumanne Juni 22, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi, akioitia nakabrasha, kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika leo Jumanne Juni 22, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akimwelekeza jambo Katibu wa NEC Oganaizesheni Moudline Castico kabla ya kuanza kikao hicho.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika leo Jumanne Juni 22, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.

©CCM Blog 2021, By: Bashir Nkoromo Chief Admin CCM Blog

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages