LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 11, 2021

CCM MKOA WA DAR YATAKA PUGU NA MSONGOLA KUPEWA WILAYA KUEPUKA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI HUDUMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Katty Slyvia Kamba akizungumza na viongozi wa CCM na watendaji mbalimbali wa Serikali katika Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kikao cha majumuisho ya kuhitimisha ziara yake na Sekretarieti ya CCM mkoa huo, Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Lamada, Ilala. 

Mama Katty Kamba amezungumzia mambo mbalimbali ytaliyojiri wakati wa ziara hiyo, ikiwemo msongamano wa wanafunzi katika madarasa na huduma hafivu za kijamii katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa wilaya hiyo.

Amesema katika maeneo ya Pugu na Msongola amekuta shule moja ina watoto zaidi ya 100 darasani, pia maeneo mengi yapo umbali mrefu kutoka zilipo shule.

" Hebu fikirieni jamani, mtoto atoke Bangalo (Kijiji) aendele kwa mguu hadi shule ya Pugu Station, na pia alazimike kuvuka mto Msimbazi,. haiwezekani," alisema Katty Kamba.

Amesema, ili kuondoa changamoto hizo kuna umuhimu wa wananchi wanaoishi Pugu na Msongola kupatiwa Wilaya yao na Halmashauri kwa sababu wapo mbali mno na ilipo Makao Makuu ya Wilaya na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma akizungumza katika kikao hicho. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Shaibu Akwilombe
Sekretarieti ya kikao ikiwa kazini kwenye kikao hicho
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Shaibu Akwilombe akizungumza katika kikao hicho.  Akwilombe amezungumza mambo mbalimbali kuhusu uhai wa chama na usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Akwilombe amewaonya wanaoendekeza makundi ndani ya Chama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Ndani ya Chama utakaofanyika mwakani.

" Ni siku chache zilizobaki kufikia kipindi cha uchaguzi mkuu ndani ya Chama utakaofanyika mwakani. Najua kipindi kama hiki baadhi ya wana CCM hujaribu kumvika taswira mbaya kwa kuwapakazia mambo ya hovyo.. Tabia hii lazima iachwe", akasema Akwilombe na kuongeza kuwa tabia hiyo licha ya kusababisha mwanachama aliyepakaziwa kuonekana mbaya lakini hukichafua pia chama.

Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Shaibu Akwilombe akisisitiza jambo wakati akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Akwilombe
Baadhi ya Viongoziwakimsikiliza Akwilombe.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mussa Kilakala akiwa kwenye kikao hicho. Wapili ni Katibu Tawala wa Ilala Charangwa Selemani.
Washiriki wa kikao hicho wakiwa ukumbini
Baadhi ya Madiwani waliohudhuria kikao hicho wakishangilia wakati Akwilombe akionya wana CCM ambao huchafua wenzao ili kupata uypenyo wa kuwania uongozi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mkoa wa Dar es SalaamYusuf Magid Nassoro akizungumzawakati wa kikao hicho.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Iddi Mkowa akizungumza kumkaribisha kuzungumza Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Katty Slyvia Kamba.
Kisha akampatia kipaza sauti
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Katty Slyvia Kamba akizungumza na viongozi wa CCM na watendaji mbalimbali wa Serikali katika Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kikao hicho. 


WAJUMBE WAKIWA KATIKA KIKAO HICHO

2
3
4
5
6
Picha zote na Bashir  Nkoromo,CCM Blog

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages