Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Katanga amezindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma Mei 6,2021.
Madhumuni ya Mkataba huo ni makubaliano kati ya mtoa huduma yaani Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wateja ikiwa ni ahadi ya kutoa huduma bora kwa wateja . Mkataba huo unaelekeza na kuanisha viwango vya huduma ambavyo wateja wanatarajia kupata ili kufikia malengo yao.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Juma Katanga (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Leonald Akwilapo (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, wakiwa na mikataba hiyo baada ya kuzindua.Katibu Mkuu, Dkt. Akwilapo akionesha mktaba baada ya kukabidhiwa.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Elimu na taasisi zake wakiwa kwenye hafla hiyo.
Naibu Waziri Katanga, akielezea umuhimu wa watumishi kuzingatia mkataba huo wakiwa kazini.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu
Waziri Katanga akizindua na kugawa mkataba huo kwa baadhi ya viongozi, Pia Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt Akwilapo na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara, Moshi Kabengwe wakifafanua vipengele vya mkataba huo
....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇