*******************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amewataka wakazi wa Nyanda za Juu Kusini kutambua na kutangaza vivutio vya Utalii vilivyomo katika maeneo yao.
Akizungumza na wakazi wa jiji hilo wakati wa Tamasha la Tulia Marathon lililofanyika jijini humo Mhe, Mary Masanja amesema sehemu kubwa ya sekta ya Maliasili na Utalii ni kuhamisha wakazi wote kuvitambua vivutio vyao vya Utalii;
“Kama sekta ya Maliasili na Utalii sehemu yetu kubwa ni kuhamasisha wanambeya, wanakanda ya nyanja za juu kusini kuvitambua vivutio walivyonavyo katika maeneo yao, sisi tunahamasisha Utalii wa ndani kupitia vivutio tulivyonavyo”
Aidha amesema kuwa nyanda za juu kusini hasa jijni la mbeya kuna vivutio vingi na hivyo inapaswa vitangwazwe kwani maeneo hayo yanahamasisha utalii wa ndani na nje ya nchi;
“Tuna Msitu wa Asili wa Rungwe ,tuna Ziwa Kingosi ,tuna Hifadhi ya Ruaha , tuna kimondo kwahiyo haya maeneo yote kwa Nyanda za juu Kusini ni maeneo mazuri ambayo yanahamasisha Utalii wa ndani na wa nje ya nchi” amesema Mary
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇