Ujenzi wa Ofisi ya Masjala ya ardhi ya Manispaa ya Iringa ukiendelea baada ya Mpango wa Kurasimisha Raisilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kupokea fedha kutoka Hazina Shilingi 978,110,300.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nshani katika Halmashauri ya Sumbawanga wakifanya kikao kujadili uendelezaji wa shughuli za ujenzi wa ofisi ya masjala ya ardhi ya kijiji hicho katika eneo ambalo ujenzi ulifikia hatua ya msingi/jamvi na sasa kamati zimeundwa kuiendeleza azma hiyo kwa kushirikiana na MKURABITA.
Wananchi wa Kijiji cha Mwakauta katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete wakiwa katika eneo lenye msingi wa jengo la ofisi ya masjala ya ardhi ya kijiji hicho linalotarajiwa kukamilishwa hivi karibuni baada ya MKURABITA kupokea fedha kutola Hazina.
Timu ya MKURABITA na wawakilishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo wakiwa katika eneo ujenzi masjala ya ardhi na baadhi ya viongozi kijiji cha Katuka mkoani Rukwa.
Wananchi na uongozi wa kijiji cha Gurungu katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi wakijadili na kuunda kamati zitakazo simamia zoezi la ukamilishaji wa jengo la ofisi ya masjala ya ardhi ya kijiji hicho kwa kushirikiana na MKURABITA na halmashauri ya Wilaya
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) imepokea kiasi cha Shilingi 978,110,300.00 kutoka Hazina kwa ajili ya ujenzi wa masjala za ardhi za vijiji 24. Aidha, ujenzi wa masjala hizi ni mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli za MKURABITA katika kurasimisha ardhi na biashara nchini.
Ujenzi wa ofisi hizi za masjala za ardhi za vijiji uko katika hatua mbalimbali ikiwemo zile zilizofikia hatua ya ukamilishaji, hatua ya jamvi na zile ambazo hazijaanza lakini tayari wananchi wameweza kukusanya vifaa vya ujenzi ikiwemo mawe, kokoto na mchanga. Kazi ya ujenzi miundo mbinu muhimu ya masjala za ardhi za vijiji ni hitaji la kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Namba 5 ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1997. Kutokana na ufinyu wa bajeti ya miradi ya maendeleo ujenzi wa masjala katika vijiji 24 haukuweza kukamilika kwa wakati, hivyo kwa serikali kutoa fedha hizo kwa MKURABITA kunaondoa mkwamo wa ukamilishaji wa ujenzi huo ambao ulianza mnamo mwaka 2010. Hata hivyo, zipo baadhi ya masjala ambazo ziliweza kukamilika katika Halmashauri za Wilaya za Handeni , Bagamoyo, Itigi, Mpwapwa, Mbarali na moja katika Shehia ya Kiungoni Wete, Pemba.
Aidha, katika ujenzi wa masjala hizi za vijiji MKURABITA huingia makubaliano na Halmashauri ya Wilaya na Kijiji husika kwa utaratibu unaohusisha kijiji /wananchi kuchangia nguvu kazi na baadhi ya vifaa ikiwemo ukusanyaji wa mawe, kokoto na maji ambapo MKURABITA huchangia gharama za vifaa vipatikanavyo nje ya eneo hilo ikiwa ni pamoja na saluji, mabati na nondo. Kwa upande wa Halmashauri jukumu lao ni kusimamia manunuzi na uthibiti wa viwango kupitia idara ya ujenzi. Katika kuhakikisha matumizi sahihi ya wazi ya pesa za ujenzi katika ngazi ya kijiji, kamati kuu tatu huundwa ambazo ni pamoja na Kamati ya ujenzi, Kamati ya manunuzi na kamati ya mapokezi ambayo inasimamia na kutoa vifaa kwa ajili ya ujenzi.
Baadhi ya Halmashauri za Wilaya zinazohusika na zoezi hili la ukamilishaji wa ujenzi wa masjala za vijiji ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Nachingwea, Makete, Rufiji, Newala, Mvomero, Kalambo, Sumbawanga, Itigi, Meru, Moshi, Mwanga na Mbinga
MKURABITA inaendelea kutekeleza mapendekezo ya maboresho ya kisheria na kitaasisi yenye lengo la kurahisisha mchakato wa urasimishaji rasilimali na biashara nchini sambamba na kuwezesha ukuzaji wa mitaji kwa wamiliki waliorasimishaji ardhi na biashara zao. Aidha, mapendekezo hayo yameainishwa katika makundi makuu matano ambayo ni a ni kurahisisha urasimishaji wa ardhi, matumizi ya kiuchumi ya rasilimali ardhi, kurahisisha urasimishaji biashara sambamba na utaratibu wa kuanzisha na kufunga biashara pamoja na mapendekezo ya masuala mtambuka .MKURABITA ambayo imeanzishwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2004 kwa Tamko la Rais la tarehe 30 Septemba 2003 ina lenga katika kuwawezesha wananchi wanaomiliki rasilimali na biashara katika mfumo usio rasmi kuingia katika mfumo rasmi ili kuwa washiriki katika uchumi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria.
Tangu kuanzishwa kwa MKURABITA, Halmashauri za wilaya 58 Tanzania Bara zimejengewa uwezo pamoja na Wilaya nne (4) za Zanziba katika masuala ya rasimishaji ardhi vijijini. Jumala ya mashamba 140,451 yamepimwa Tanzania Bara, ambapo Zanzibar Hati za matumizi ya ardhi 504 zimeandaliwa na kutolewa kwa wamiliki wa maeneo hayo. Pia masjala mbili (2) za wilaya na 27 za vijiji zimejengwa na kukamilika ikiwemo jengo la Afisi ya Shehia ya Kiungoni, Wete, Pemba. Katika utaratibu huu wa kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, MKURABITA imeweza kuvifikia vijiji 559 ambapo Halmashauri 58 zimeendeleza kazi za urasimishaji katika vijiji 224 kwa kushirikiana na MKURABITA na vijiji 335 vimefikiwa na Halmashauri zenyewe baada ya kujengewa uwezo na MKURABITA kwa kupatiwa mafunzo na vifaa vya urasimishaji.
Kwa upande wa urasimishaji ardhi mijini, MKURABITA imejenga uwezo na kutoa vifaa katika Halmashauri za Miji, Manispaa na miji 10 kwa Tazania Bara na Wilaya nne (4) za Tanzania Zanzibar. Jumla ya viwanja 10,977 vimepimwa na hati miliki 2,233 zimeandaliwa na kutolewa kwa wamiliki. Pia kuna mashamba 742 ambayo yamepimwa kwa kutumia Sheria ya Ardhi Namba 4 katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na uandaaji wa Hati miliki unaendelea. Aidha, Zanzibar kuna viwanja 4,600 vimepimwa na Hati za matumizi ya Ardhi 63 ziliandaliwa na kutolewa kwa wamiliki wa maeneo husika.
Aidha, katika kutekeleza mapendekezo ya maboresho ya kisheria na kitaasisi yaliyoasisiwa na MKURABITA, imebuni utaratibu unaorahisisha urasimishaji biashara kwa kutumia vituo jumuishi vya urasimishaji na uendelezaji wa biashara na uwekezaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Jumla ya vituo 13 vimeanzishwa ikiwemo kituo kimoja kilichopo Darajani, Unguja na; vituo vinne ujenzi wake unaendelea .
Hivi karibuni, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) imepokea kiasi cha Shilingi 978,110,300.00 kutoka Hazina kwa ajili ya ujenzi wa masjala za ardhi za vijiji 24. Aidha, ujenzi wa masjala hizi ni mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli za MKURABITA katika kurasimisha ardhi na biashara nchini.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇