Mratibu wa Taifa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani. |
RAIS
mstaafu wa Awamu ya Nne nchini Tanzamia, Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa
kufungua mkutano wa kimataifa wa elimu Bora ulioandaliwa na Mtandao wa
Elimu Tanzania (TEN/MET) ambao utashirikisha wadau mbalimbali wa elimu
kutoka serikalini, asasi na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya
nchi.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari, Mratibu wa Taifa
TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga amesema mkutano huo wa kimataifa juu ya elimu
bora unatarajiwa kufunguliwa na Rais mstaafu Awamu ya Nne, Kikwete
siku ya Jumanee ya tarehe 18 Ukumbi wa Kisenga Jengo la LAPF na
utafanyika hadi tarehe 20 Mei 2021.
Bw.
Wayoga alisema Mkutano huo wa Ubora wa Elimu utajadili Uwajibikaji wa
pamoja katika kugharamia elimu bora nchini, ambapo utatoa fursa kwa
wadau wa elimu ikiwepo serikali, wanachama wa mtandao, Washirika wa
Maendeleo (Development Partners) pamoja na wadau mbalimbali wa elimu
nchini kujadili hali ya ubora wa elimu kwa nia ya kuboresha zaidi.
Aidha
aliwataja baadhi ya washiriki wa Mkutano huo ni pamoja na wajumbe
kutoka Wizara ya Elimu, SayansinaTekinolojia, TAMISEMI,Mashirika yasiyo
ya kiserikali, Wadau wa maendeleo, waheshimiwa Wabunge, Taasisi za elimu
ya juu, tasisi za utafiti, Vyuo na shule za ufundi, Walimu, Wazazi na
Wanafunzi.
“…mkutano
huu utahudhuriwa pia na mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao, wageni
wengine mbalimbali kutoka nchi za ng’ambo, makampuni na taasisi za watu
binafsi. Wajumbe takriban 200 wamethibitisha kushiriki katika mkutano
huu; baadhi watakuwa wakishiriki kwa njia ya Mtandao,” aliongeza Mratibu
wa Taifa TEN/MET, Bw. Wayoga.
Alibainisha
kuwa pamoja na mambo mengine Mkutano huo unatarajiwa kutoka na maazimio
ambayo ni mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya elimu hapa nchini kwa kutumia matokeo ya taarifa
za tafiti na uzoefu kutoka nchi nyingine.
“…Maandalizi
yote yamekamilika hivyo naomba kuwashukuru wadau mbalimbali ambao
wamewezesha kufanyika kwa Mkutano, ubalozi wa Swedeni , Global
Partnership for education kupitia mradi wa Education Out Loud, Norad
kupitia Action Aid Tanzania, Pestalozzi na HDIF Tanzania.” Alisema
kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇