LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 2, 2021

RAIS DKT.MWINYI TUTAZITATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI ILI WATEKELEZE MAJUKUMU YAO VYEMA

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Maadhimishi ya Siku ya Wafanyakazini Duniani Mei Mosi yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.


Na Mwashungi Tahir ,Maelezo   

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema  Serikali ina malengo mazuri  ya kuzitatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi ili kutekeleza  vyema majukumu yao.

Hayo ameyasema leo huko katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil huko Kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa sekta mbali mbali wakiwemo wa Serikali na binafsi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo huadhimishwa duniani kote.

Amesema Serikali inathamini na kutambua mchango muhimu  wa wafanyakazi katika kufikia harakati za maendeleo na  utekelezaji mzuri na kuhakikisha kuwa iko wazi kwa ajili ya kuwatumikia wafanyakazi wake.

Amefahamisha kuwa  Serikali ina dhamira njema kwa watumishi kwani imeandaa mazingira mazuri  kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi katika nyanja zote za uchumi na katika kujipatia maendeleo .

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Kazi, Uchumi na Uwekezaji  Mudrik Ramadhani Soraga amesema wizara yake ina mshirikiano makubwa na Shirika la Kazi  duniani (ILO) kwani imesaidia kutoa mafunzo kwa vijana wapatao 200 na kujipatia ajira.

amesema janga la corona bado linaathiri wafanyakazi katika kukwamisha maendeleo na pia kuathiri uchumi wa Nchi na hivyo wizara itaendelea kushirikiana na vyama shirikisho kuona hali inaimarika kwa kila sekta katika utendaji wa kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa shirikisho wa vyama vya wafanyakazi Mwatum Khamis Othmani akisoma risala amesema bado kuna baadhi ya watendaji wenye nyadhifa za juu hujifanyia marekebisho katika mishahara yao na kuwadhalilisha wafanyakazi wa chini.

Siku hii ya maadhimisho kwa wafanyakazi hufanyika kila mwaka Duniani kote ambapo kauli mbiu ya mwaka huu  ni Uwajibikaji na haki ndio msingi wa maendeleo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages