LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 4, 2021

NDUGULILE ATAKA USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KATIKA KUELEKEA UCHUMI WA KIDIJITALI

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile (Mb) ameitaka sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuleta mapinduzi ya TEHAMA kwa lengo la kuelekea uchumi wa kidijitali.


Dkt Ndugulile aliyasema hayo aliposhiriki kwenye mkutano kupitiq mtandao (Zoom meeting)  na watendaji wakuu wa makampuni binafsi kupitia umoja wao  (CEOrt).


Dkt Ndugulile aliwaeleza kuwa Serikali inaendelea kuwekeza kwenye mazingira wezeshi ya kukuza sekta ya TEHAMA na katika kuelekea uchumi wa kidijitali. Dkt Ndugulile ameitaka Sekta binafsi kusaidiana na Serikali katika kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani, kuwekeza kwenye viwanda vya vifaa vya TEHAMA na kusambaza mawasiliano katika maeneo ya pembezoni.


CEOrt kupitia kwa Mwenyekiti wao Bw Sanjay Rughani wameahidi kushirikiana na Serikali katika kuleta mapinduzi makubwa ya TEHAMA hapa nchini na wameahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali pale watakapohitajika.


Mkutano huo umeudhuriwa na Watendaji Wakuu wa Makampuni binafsi wapatao 50.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages