LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 19, 2021

MWAKANG'ATA ATAKA UJENZI UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA UANZE, BARABARA YA KIBAONI HADI MLOWO ITIWE LAMI+video

 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata ameishauri serikali kuharakisha malipo ya wakandarasi nchini ambao wanaidai serikali baada ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu nchini. 

 

Pia Mbunge Mwakang'ata ameiomba serikali kuanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga Mjini ambao umetelekezwa licha ya kulipa fidia walioupisha ujenzi. Aidha mbunge huyo ameiomba serikali kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni-Majimoto hadi Mlowo kutokana na umuhimu wake kiuchumi. 

 

 Mwakanga'ata alitoa ushauri huo alipokuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakati wa Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kikao cha 30 jijini Dodoma Mei 18, 2021. 

 

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Mwakang'ata akitoa ushauri wake huo..... 

 

 Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages