LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 26, 2021

MKURABITA KUWAPATIA MAFUNZO YA KUWAINUA KIUCHUMI ZAIDI YA WANAKIJIJI 300 WA LUGODALUTALI MUFINDI+video


 Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu (kushoto) akiwaelekeza maofisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Mufindi jinsi ya kujaza dodoso kwa kutumia mfumo wa kukusanya taarifa wa Kobo wakati wa kikao cha maandalizi ya mafunzo kwa wanufaika wa Mkurabita wa Kijiji cha Lugodalutali yatakayofanyika Jumanne ijayo Juni Mosi, 2021.Kulia ni Afisa Kilimo, Mwamini Mwakyaka na Afisa Ushirika Pili Mwaipaja.

Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Leonard Jaka akichangia hoja wakati wa kikao hicho cha maandalizi.
Afisa Maendeleo wa Halmashauri hiyo, Joha Kambala akielezea jinsi atakavyotoa elimu katika mafunzo hayo.
Temu akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho cha maandalizi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


 Na Richard Mwaikenda, Mufindi.

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) umeandaa mafunzo ya kuwainua kiuchumi zaidi ya wanufaika 300 wenye Hati miliki za kimila za ardhi zao katika Kijiji cha Lugodalutali wilayani Mufindi, mkoani Iringa. 

 Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi kilichofanyika mjini Mafinga Mei 25, 2021, Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu amesema kuwa mafunzo hayo yatafanyika Jumanne ijayo Juni Mosi katika kijiji hicho ambapo yatakuwa mafunzo ya wazi kwa wananchi wote. 

Amesema kuwa licha kuwafundisha jinsi ya kutumia hati miliki zao kuzitumia kama dhamana ya kupatia mikopo benki na taasisi zingine za fedha, pia watapata mafunzo kutoka kwa wataalamu jinsi ya kuthaminisha mali zao, kanuni bora za kilimo, faida za kujiunga na ushirika, jinsi ya kuweka kumbukumbu za mahesabu za miradi yao na kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya halmashauri. 

Katika mkutano huo watakuwepo watalaamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, maofisa wa Benki watakaoelezea kuhusu faida za mikopo lakini pia wananchi wataruhusiwa kufungua akaunti za chap chap wakati mafunzo hayo.

 Vile vile atakuwepo mtaalamu wa masuala ya ufugaji wa nyuki kibiashara hasa kutokana na msaada wa mizinga 30 utakaotolewa na Mkurabita katika Kijiji hicho. 

Mdau nakuomba uendeee kusikiliza clip hii ya video, upate ufahamu zaidi yatakayojiri kwenye mkutano huo.... Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 

0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages