Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji. Mbunge wa Chemba Mohamed Moni ameeleza uhalisia wa hali ya maji katika Wilaya ya Chemba na kuiomba serikali ije na majibu ya kwanini hawakutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Farkwa.
Aidha, mbunge huyo anaewapambania wananchi wake ameeleza udhaifu wa kitengo cha manunuzi cha wizara ambacho amedai kinachukua muda mrefu kukamilisha ununuzi wa mahitaji ya vifaa vya ujenzi.
Moni pia ameiomba wizara imalizie miradi ya maji ya vijiji vya Machiga, Mapango na Chandama ambayo imesimama tangu mwaka 2014. Hata hivyo ameeleza masikitiko makubwa juu ya uchakavu wa miundombinu ya maji wilayani Chemba.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Mboni akiwapambania bungeni wananchi wake kuhusu maji....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇