LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 8, 2021

GERSON MSIGWA: TANZANIA HAKUNA WAFUNGWA WA KISIASA

Msemaji Mkuu wa Serikali
Gerson Msigwa.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, amewataka Watanzania kupuuza taarifa zilizorushwa na Televisheni moja kwamba Rais Samia Suluhu ameagiza wafungwa wa kisiasa nchini kuachiwa huru.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Msigwa amesema, taarifa hiyo haina ukweli wowote na Mheshimiwa Rais hawezi kuingilia uhuru wa Mahakama.


“Mheshimiwa Rais hajazungumza kitu chochote kuhusiana na wafungwa wa kisiasa, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa," amesema.


Msigwa amesema kuwa  kupitia video fupi inayosambaa kueleza taarifa hiyo pia imeeleza kuwa, Mheshimiwa Rais amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwaachia wafungwa hao wanaodaiwa 23 ambao hawapo.


“Mheshimiwa Rais haingilii uhuru wa Mahakama pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali haendeshi masuala kama haya ya mahakamani kwa mujibu wa sheria zetu na taratibu zetu hivyo Watanzania wapuuze taarifa hizo hazina ukweli wowote,"amesisitiza.


Msigwa amesema, mpaka sasa Serikali imeanza kuchukua hatua na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi, Kenya inachukua hatua kufuatilia kwa nini chombo hicho kimepotosha kiasi hicho.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages