Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Muhambwe Dk. Florence Samizi, akionyesha Hati yake ya ushindi wa Ubunge wa jimbo hilo, baada ya kukabidhiwa rasmi hati hiyo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Diocles Rutema, wakati msimamizi huyo akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo mdogo uliofanyika jana.
Dk. Samizi ameshinda Uchaguzi huo baada ya kupata kura 23,44I kati ya kura 35,339 sawa na asilimia 68 akifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Masabo Julius aliyepata kura 10,847 na Mgombea wa Democratic Party (DP) Philipo Fumbo aliyepata kura 368.
Baadhi ya Viongozi wa CCM wakishangilia pamoja na Dk. Samizi baada ya matokeo kutangazwa. Aliyemuinua mkono Dk. Samizi ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Erasto Sima.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe Marycelina Mbehoma akikabidhi Cheti cha ushindi mshindi wa kiti cha Ubunge Jimbo la Buhigwe Mkoani Kigoma, Kavejuru Felix wa Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuibuka mshindi na kuwabwaga wapinzani wake 12 alioshiriki nao katika Uchaguzi mdogo uliofanyika jana, Mei 16, 2021.
Felix ameibuka kidedea baada ya kupata kura 25,274 Kati ya kura 30,320 halali zilizopigwa, huku
Mgombea wa ACT Wazalendo Garula Kudra akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 4,749 na nafasi ya tatu ikienda kwa Abdallah Bukuku wa Chama cha CHAUMA aliyepata kura 125.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇