LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 6, 2021

BAJETI YA WIZARA YA MAJI 2021/22 SH. BILIONI 680.3, WAZIRI AWESO ASEMA KIWANGO CHA UPATIKANAJI MAJI MIJINI NA VIJIJINI KIMEONGEZEKA

Waziri wa Maji Juma Aweso akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, Bungeni jijini Dodoma, leo.


Bungeni, Dodoma

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewasilisha  Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22 ya kiasi cha jumla ya Sh. Bilioni 680.3, Bungeni jijini Dodoma, leo.


Akiwasilisha bejeti hiyo Waziri Aweso ameeleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya maji katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021 kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa huduma za maji nchini kutoka asilimia 70.1 vijijini na 84 mijini mwaka 2019/20 hadi asilimia 72.3 vijijini na 86 mijini.


Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa idadi ya maabara za ubora wa maji zenye ithibati kutoka moja ya Mwanza hadi kufikia saba, kuzinduliwa kwa miradi mikubwa ya maji ya Tabora – Igunga - Nzega pamoja na Isaka Kagongwa baada ya  utekelezaji kukamilika. Aidha kukamilika kwa utekelezaji wa kihistoria wa miradi 422 ya maji ambapo kati ya hiyo ya vijijini ni miradi 355 na mijini miradi 67.


Waziri Aweso amesema hivi sasa   kasi na ubora wa utekelezaji wa miradi ya maji imeongezeka  na  gharama za ujenzi zimepungua kutokana na kutumia utaratibu wa force account. 


Mafanikio mengine ni pamoja na kuanza kutoa huduma ya maji kwa miradi 85 iliyokuwa na changamoto baada ya kufanya mabadiliko makubwa katika utaratibu wa usimamizi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages