LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 25, 2021

WABUNGE VITI MAALUMU KUMUONA RAIS SAMIA AWASAIDIE WASINYANYASWE, WASITISHIWE MAJIMBONI


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma kupitia tiketi ya CCM, Jacqueline Msongozi amepaza sauti bungeni akilalamikia kitendo cha wabunge wa viti maalumu kunyanyaswa kijinsia, kunyanyapaliwa na kufanyiwa ukatili na vitisho juu na wabunge wa majimbo wanapowajibika kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.

Msongozi aliyasema hayo alipokuwa akichangia bungeni mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo ameiomba serikali  kufanya suluhu ya jambo hilo na kwamba wanapanga kwenda kumuona Rais Samia Suluhu Hassan mara atakapopitishwa na Mkutano Mkuu wa  CCM  kuwa Mwenyekiti ili awasaidie wawe wanafanya kazi zao kwa uhuru.


Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video, Mbunge Msongozi akielezea masahibu hayo....


 Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages