Na Antar Sangali, Zanzibar
Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Kaskazini Unguja umesema sasa ni wakati muhimu kwa wanaharakati wa masuala ya Wanawake, Wanasiasa Wasomi na Makundi Maalum kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kitendo cha kupatikana kiongozi mwanamke na kuwa rais kihahitaji kushangiliwa kwa shangwe la nguvu, ari na ujasiri.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Kaskazini Unguja Maryam Muharram Shomari akiwa Mahonda mkoa Kaskazini Unguka aliyesema ni fahari kwa Mama Samia kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania.
Maryam amesema kumpata Rais Samia kuwa Mkuu wa nchi, kuzidishe mshikamano miongoni mwa wanawake viongozi wa kisiasa , madiwani, wawakilishi, wabunge na wanaharakati
Amesema huu ni muda muafaka wa kumuunga mkono Rais huyo kwa shangwe na vitendo vitakavyodhihirisha umoja na maendeleo .
Mary amesema bila kujali ni vyama gani au makundi yepi ya kiharakati ,itikadi za kisiasa ziwekwe kando na wanawake wamlinde na kumtetea Rais huyo
Ameeleza bila kujali makundi ya wanasiasa wanawake au wasomi waanze kujadili vikwazo na chamgamoto zinazowakabili wanawakw kitaifa na kikanda.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema iwapo wanawake watautumia vyema wakati kwa kushikamana, kuzidisha juhudi ,bidii na maarifa, watawanusuru wanawake walioko mijini na vijijini
Amewataka wanawake wenzake kila mmoja kwa wakati wake kuwa askari dhamana atakayelinda kiti cha urais wa mama samia kwani dhamana hiyo ni dhamana ya wanawake wote.
Maryam amengeza kusema kuwa itakuwa fedha ikiwa wanawake watasita kumtetea mwanzao ataposakamwa na watetea wa mifumo kandamizi badala yake wote wasimame kidete
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa uwt mkoa kaskazini unguja amesema uamuzi Tanzania kumpata rais mwanamke ufunhue njia kwa afrika hatimaye kila nchi ifikirie na kuwaamini wanawake
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇