Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo April 11,2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Entebbe, Rais Samia atafanya mazungumzo ya faragha na Museveni na kisha Viongozi hao watahudhuria hafla na kushuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇