LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 3, 2021

RAIS SAMIA AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge aliyeambatana na viongozi wenzake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akitokea Jijini Dodoma leo tarehe 03 Aprili 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe pamoja na viongozi wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akitokea Jijini Dodoma leo tarehe 03 Aprili 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam wakati akiondoka uwanjani hapo mara baada ya kuwasili leo tarehe 03 Aprili 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili leo tarehe 03 Aprili 2021 wakati akitokea jijini Dodoma. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages