LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 17, 2021

RAIS SAMIA ATEUA KATIBU WA RAIS, NA WASAIDIZI WANANE KATIKA OFISI BINAFSI YA RAIS

Rais Samia Suluhu Hassan

Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, amemteua Juma Selemani Mkomi kuwa Katibu wa Rais (KR) na kueleza kuwa uteuzi huo umeanza Machi 29, 2021.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu kutoka jijini Dodoma jana usiku, imesema, pia Rais Samia amefanya uteuzi wa Wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) kama ifuatavyo;

Said Ali Juma (Mnikulu), Balozi Dk. Mussa Julius Lulandala (Nyaraka na Ukalimani -PAP-TD), Balozi Ali Bujiku Sakila (Hotuba - PAP-SD) na Maulidah Bwanaheri Hassan (Diplomasia- PAP-DA).

Wengine ni Felister Peter Mdemu (Maendeleo ya Jamii), Nehemia Ernest Mandia (Sheria- PAP-LA), Dk. Blandina Kilama (Uchumi- PAP-EA) na Dk. Salim Othman (Siasa- PAP-PA).

Taarifa hiyo imesema uteuzi wa Wasaidizi hao wa Rais unaanza jana, Aprili 16, 2021.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages