LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 22, 2021

MTEMVU ATOA SADAKA YA CHAKULA KWA AJILI YA MFUNGO WA RAMADHANI

Mkurugenzi wa kampuni ya Bravo Agency, Abbasi Mtemvu, akiwakabidhi msaada wa vyakula watu wenye ulemavu, Dar es Salaam, jana. (Na Mpigapicha Wetu).


Na Mwandishi Maalum

Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravo Agency Abbasi Mtemvu, ametoa msaada wachakula kwa watu wenye ulemavu, ili kiwasaidie katika Mwezi Mtufuku wa Ramadhani.


Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Temeke, amekabidhi msaada huo leo, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kawaida yake kila inapofika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa makumdi mbalimbali ya watu wenye uhitaji maalumu.


Chakula hicho kinahusisha unga wa ngano, sembe, sukari, mafuta ya kupikia na tende.


Akikabidhi msaada huo, Mtemvu alisema amekuwa akitoa msaada kila ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakati wa Sikukuu za Krismas ili kuisaidia jamii yenye mahitaji maalumu.


"Hii imekuwa ni kawaida yangu kutoa sadaka.Tangu  nikiwa Mbunge wa Jimbo la Temeke na sasa sio Mbunge lakini naendelea kutoa kila ikifika wakati huu na Krismass," alisema Mtemvu.


Alisema  pia ataendelea kutoa  msaada kwa vituo vya watoto yatima ili  kuwapa mahitaji muhimu hususan chakula.


Alisema ni vizuri kuwasaidia watu hawa wenye mahihitaji maalumu ili na wao wajione sehemu ya jamii, watu wenye uwezo wa kutoa msaada na wao wakasaidia watu hao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages