Na Mwandishi huru, Morogoro
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emanuel Kalobelo amezielekeza Halmashauri zote mkoani hapa, kuwatumia wataalam kutoka Chuo Cha Ardhi Morogoro katika kutatua migogoro ya ardhi.
Mhandisi Kalobelo ameyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha Ardhi Morogoro, akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mhandisi Kalobelo ameongeza kwamba ni aibu kwa Mkoa wa Morogoro kuwa na migogoro mingi ya Ardhi ilihali Chuo Kinachozalisha wataalamu wa upimaji na mipango miji kipo Mkoani humo.
Mapema Mkuu wa Chuo hicho Huruma Lugalla katika hotuba yake amesema Chuo kitaendelea kutoa elimu bora ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi, kuongeza vifaa vya vya upimaji, uchoraji pamoja na vifaa vya TEHAMA ili wanafunzi waendane na kasi ya teknolojia.
Mahafali hayo yalitanguliwa na Kikao cha Bodi kilichofanyika siku moja kabla ambapo Mwenyekiti wa Bodi Professor Mpanduji alipongeza uongozi wa chuo kwa kuchukua hatua na kuongeza kasi ya upimaji baada ya kupata ripoti ya kuoima viwanja zaidi ya 19,000 ndani ya miezi miwili.
**
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emanuel Kalobelo, akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro Huruma Lugalla Kitabu cha njia mbadala ya kumaliza migogoro ya arhi, wakati wa mahafali hayo.
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emanuel Kalobelo akizungumza kwenye mahafali hayo.Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emanuel Kalobelo akionyeshwa baadhi ya mashine za kupimia
Brass band ikiongoza msafara wa maandamano kuingia eneo la magafali hayo.
Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emanuel Kalobeloakiwa katika picha ya pamoja uongozi wa chuo na wahitimu.
Brass band ikiongoza msafara wa maandamano kuingia eneo la magafali hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇