LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 5, 2021

GERSON MSIGWA ATEULIWA NA RAIS SAMIA KUWA MKURUGENZI WA MAELEZO NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI



Gerson Msigwa


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali.


Kulingana na Uteuzi huo uliotangazwa jana, Aprili 4, 2021, Msigwa anachukua nafasi ya Dk. Hassan Abbas Said ambaye katika uteuzi huo, ameteuliwa na Rais Samia kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Msigwa alithibitisha na aliyekuwa  Rais Hayati Dk. John Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Jumatano Agosti 31, 2016. 


Kabla ya uthibitisho huo, Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo hicho katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015 Wakati wa Uongozi wa Rais wa awamu ya Nne, ambaye sasa ni Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.


Kabla ya Gerson Msigwa kwenda kufanyakazi Ikulu, alikuwa Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Televisheti ya Taifa (TBC) ambaye alikuwa akiripoti kutokea Songea mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages