LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 22, 2021

DIWANI LUCA WA KATA YA MSASANI AMWAGA MILIONI 10 UJENZI WA MITARO

Na Mwandishi Maalum

Diwani wa  Kata ya Msasani, Kionondoni, Jijini Dar es Salaam, Luca Neghest,  amesema   dhamira yake ni kuona  wananchi wa Kata hiyo  hasa wanaoishi katika Mitaa ya Mikoroshini na Bonde la Mpunga wanaondokana na changamoto kubwa ubovu wa  za miundo mbinu  hususan barabara na mitaro.


Luca amesema katika kufanikisha hilo tayari amepata Mkandarasi Kampuni ya Nzinga Constructions and Plumbering Limited ambaye ameanza kufumua  kabisa  mitaa hiyo ili kujenga miundombinu ya kisasa  hasa ya mifereji na mitaro  katika barabara.


 Anaeleza ujenzi huo  unagharimu zaidi ya sh. milioni 10 ambazo  anagharimia zikiwa ni fedha zake mfukoni.


“Najitolea  kwa nguvu zangu mwenyewe  kwa sababu wananchi katika mitaa hii wameishi kwa adha kubwa iliyo watesa kwa kipindi kirefu,”anaeleza  Diwani Luca.


Anasema, baada ya kuona adha ya mafuriko  waliyokuwa wakiipata wananchi wa Msasani  hususan Bonde la Mpunga na Mikoroshoni, aliamua kumtafuta mkandarasi mzalendo Nzinga ili kuona namna gani watashirikiana kuwaokoa wananchi.


“Nashukuru Nzinga walikubari kutusaidia  hivyo ujenzi huu wa mifereji, kuweka makavati  katika maeneo korofi  ni wa kujitolea na gharama yake ni zaidi y ash. milioni 10 ambazo  nimegharamia, anaeleza diwani huyo.


Anasema maendeleo katika kata hiyo si kwa mitaa hiyo bali Kata  nzima ya Msasani inayohusisha pia mitaa ya Masaki na Oysterbay.


“Tumeanza na mitaa ya Mikoroshoni na Bonde la Mpunga, lakini nitagusa maeneo yote ya Kata ya Msasani ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto,” ameeleza Diwani huyo.


Mhandisi wa Kampuni ya Nzunda ,  Jordan Mbaga,  alisema kazi  ya kuweka makarabati inaendelea kwa kasi na imefikia asilimia 12.


“Dhamira  ni kudhibiti maji  yasiingie katika nyumba za watu bali yafuate mkondo.Tutajenga  mfereji  hadi Bahari ya Hindi,”ameeleza  Mhandisi Mbaga.

Diwani wa  Kata ya Msasani, Kionondoni, Jijini Dar es Salaam, Luca Neghest, akipata maelezo alipotembelea kuona hali ya mitaro na barabara katika Kata hiyo, leo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages