LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 6, 2021

ASKOFU BUNDALA WA KANISA LA PHAMT BETHANIA ALA CHAKULA NA WATOTO WANAOISHI MITAANI DODOMA, AWAHUBIRIA INJILI+video

Emmanuel Bundala (aliyevaa koti jekundu) akiungana na watoto wanaoishi mitaani kula chakula cha mchana kilichoandaliwa na Kanisa la Pentekoste  la PHAMT Bethania Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere Square. Emmanuel ni mtoto wa Askofu Bundala ambaye alishiriki kuwakusanya watoto hao pamoja maandalizi ya chakula hicho. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Askofu Julius Bundala wa Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethenia Dodoma  akiwahubiria watoto wanaoishi mitaani baada la kula nao chakula cha mchana siku ya Jumatatu ya Pasaka kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dodoma.
Watoto wanaoishi mitaani wakinawishwa mikono tayari kupata chakula

Wakigawiwa chakula

Sasa ni wakati wa kula







Mtoto anayeishi mitaani  Joseph Jailos(17)  akielezea jinsi alivyotoka Kigoma hadi kwenda Dodoma ambako hadi sasa anaishi mitaani.
Mtoto anayeishi mitaani  Godfrey John Bosco (15) aliyeishia darasa nne  katika Shule ya Msingi Majengo mkoani Kigoma, akielezea jinsi alivyotoka Kigoma hadi kwenda Dodoma ambako hadi sasa anaishi mitaani.
Mtoto anayeishi mitaani, aliyejulikana kwa jina la Athuman kutoka mkoani Kigoma, akielezea mahasibu mbalimbali wanayopata wanapotafuta riziki mitaani.
Emmanuel Bundala mtoto wa Askofu Julius Bundala wa Kanisa hilo, akielezea lengo la kuwaandalia chakula watoto hao. Kwa habari zaidi sikiliza kupitia clip ya video hapo chini.. 
Askofu Bundala (kulia) akiwa na baadhi ya watoto wanaoishi mitaani pamoja na familia yake  baada ya kupata mlo.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Askofu Julius Bundala wa Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethenia Dodoma akiwahubiria watoto wanaoishi mitaani baada ya kula nao chakula cha mchana siku ya Jumatatu ya Pasaka kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dodoma.

Baada chakula aliwahubiria kwa kuwataka kumrudia Yesu Kristo ili warudi kwenye hali yao ya kawaida badala ya kuishi maisha yasiyofaa mitaani.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video, Askofu Bundala, mwanaye Emmanuel wakielezea lengo la kuwasaka watoto hao na kula nao chakula pamoja na kuwahubiria neno la Mungu lakini pia utawasikiliza watoto wakielezea pamoja na mambo mengine na jinsi wanavyopatwa na maswahibu wanapoishi mitaani....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages