Mar 3, 2021

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA, AWAONYA VIONGOZI WA VIJIJI

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa Kata ya Rudi, Jimboni kwake, Wilayani Mpwapwa, leo, ambapo amewataka wananchi wa Kata hiyo kutunza mazingira kwa kutofanya shughuli za kilimo au kukata miti milimani jimboni humo. Pia amewaonya Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na waharibifu wa mazingira katika maeneo hayo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akiingia katika darasa la shule ya msingi Rudi, lililojengwa mwaka 1950 katika Kata ya Rudi, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa. Aliiagiza darasa hilo likarabatiwe bila kubadilishwa muonekano wake. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa Kata ya Rudi, Jimbo kwake, Wilayani Mpwapwa, leo, ambapo amewataka wananchi wa Kata hiyo kutunza mazingira kwa kutofanya shughuli za kilimo au kukata miti milimani jimboni humo. Pia amewaonya Watendaji wa Vijiji wanaoshirikiana na waharibifu wa mazingira katika maeneo hayo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Rudi iliyopo katika Kata ya Rudi, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa, leo, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kukagua madarasa yanayojengwa katika shule hiyo kongwe iliyojengwa mwaka 1950. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages