LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 22, 2021

UTOAJI HESHINA ZA MWISHO KITAIFA KWA MWILI WA DK. MAGUFULI UWANJA WA JAMHURI JIJINI DODOMA, NAO WAGUBIKWA NA HUZUNI NA VILIO KAMA DAR

 


Pole Mama yetu, Pole Sote: Mama Janeth Magufuli ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli akiwa mwenye huzuni na majozi yasiyomithilika, wakati wa kuagwa Kitaifa Mwili wa Dk. Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, leo.

Umati wa wananchi waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia Msafara uliokuwa ukipeleka Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma Mwili wa aliyekuwa Rais wa tanzania Dk. John Magufuli kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho Kitaifa, leo
Msafara uliokuwa na Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli ukiingia Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho Kitaifa, leo

Wananchi wakiwa wamefurika katika Uwanja wa jamhuri Kutoa heshima zao za mwili kwa mpendwa wao JPM

Na CCM Blog, Dodoma

Maelfu ya wananchi, Marais wa nchi 17, Mjane Mama Janeth Magufuli na viongozi  mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo Viongozi Wastaafu wastaafu wote wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,  wamefika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk.John Magufuli ambaye amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu kutokana na maradhi ya moyo katika mfumo wa umeme.



Wingi wa wananchi waliojumuika kwenye barabara za jiji la Dodoma wakiimba ‘Jeshi Jeshi Jeshi, Rais Rais Rais, Baba Baba Baba, Magu Magu Magu huku wengine wakilia ni uthibitisho tosha kuwa Dk Magufuli alikuwa kipenzi cha watanzania na wana-Dodoma.


Huzuni,Majonzi, vilio na simanzi  vilianza kutawala Bungeni kwa Wabunge kuangua vilio na Simanzi wakati wakitoa heshima zao za mwisho za kumuaga Dk. Magufuli mara baada ya hapo mwili uliwasili  katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo uwanja huo ulilipuka kwa  Vilio na Simanzi kwa wananchi na viongozi waliofika.


Uwanjani maelfu ya wananchi, viongozi mbalimbali kutoka nje ya Tanzania walianza kujitokeza mapema alfajiri ya leo Machi 22, 2021 ambao waliokuwa wametoka maeneo mbalimbali na wote wakiwa na hamu ya kushuhudia shughuli mbalimbali za kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk.Magufuli ambaye kwenye uongozi wake aliamini katika kuwasadia na kusikiliza wananchi wanyonge wenye changamoto mbalimbali za kimaisha.


Mwili wa Dk.Magufuli ulifikishwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma saa 4:43 asubuhi baada ya kutoka bungeni ambapo wabunge walitoa heshima zao za mwisho kumuaga Dk. Magufuli  kabla ya wananchi na viongozi kutoka nchi mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho katika uwanja huo.


Pamoja na hayo kabla ya wananchi wakiongozwa na Rais Samia pamoja na Marais 17 kutoka mataifa mbalimbali ambapo walikuja kutoa heshima zao za mwisho Kitaifa zilizofanyika hapa Dodoma Ibada maalum imefanyika Uwanjani hapo na wakati wa Ibada hiyo mengi yamezungumzwa kuhusu Dkt.Magufuli.


Ili kuwapa fursa wananchi katika kumuaga Chuma wa Afrika mwili huo utazunguka mara tano katika Uwanja wa Jamhuri mara baada ya hapa utapitishwa katika mitaa maarufu iliyopo jijini Dodoma ambapo wananchi watajipanga kutoa heshima zao za mwisho.


Jeneza lenye mwili  wa Dk. Magufuli litapitishwa na wananchi watatoa heshima zao za mwisho kwa kumuaga watajipanga katika Uwanja wa Jamhuri,Round about ya Bahi Road Via Shule ya msingi Uhuru,Iringa Road Via Mirembe Hospital,Barabara ya Kigamboni Via Kitto Bar na Central Police, Round about ya Jamatini,Barabara ya Bunge,Emmaus ya Pili mpaka Mataa,Barabara ya Mataa kuelekea kwa Waziri Mkuu/African Dream,African Dream kuelekea njia panda ya Wajenzi,Njia panda wajenzi kuelekea Airport.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages