Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma-Miundombinu, Mhandisi Happiness Mgaalula akisoma ajenda mbalimbali wakati wa kikao hicho.
Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwenye kiao hicho
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dodoma,Mhandisi Leonard Chimagu akijibu maswali pamoja na kufafanua mambo mbalimbali kuhusu hali ya barabara mkoani humo.
Mhandisi wa Matengenezo Tanroads, Salome Kabunda akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akiuliza swali na kutaka ufafanuzi wa hali ya barabara wilayani kwake.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa akihoji utalaamu alio nao kiongozi anayesimamia uwekaji viraka kwenye barabara, kwani kila vikiwekwa huharibika haraka.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akiwa na wajumbe wengine kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa DC,Abdalah Maguo akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa Mji, Mohamadi Kiberenge
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe akit
Afisa Mkazi Madini Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Nchangwa Marwa akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Afisa Uhamasishaji Uwekezaji wa Kanda,Juma Nzima
Mbunge wa Viti Maalumu, Kunti Majala akichangia kuhusu uboreshaji wa barabara pamoja na kuunga mkono mjadala wa TARURA kuongezewa bajeti ili ifanye kazi kwa ufasaha kujenga na kuzifanyia matengenezo barabara za mijini na vijijini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa akiiomba Tarura kujenga kwa lami kipande cha barabara mita 750 kiichopo Kondoa mjini.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba, Zahara Michuzi (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, wakati wa kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Kessy Maduka akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mahenge akisisitiza jambo alipkuwa akifunga kikao hicho.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge ameagiza viongozi wa ngazi mbalimbali wa mkoani humo, kwenda kusimamia vyema ujenzi wa miradi ya barabara unaoendelea maeneo mbalimbali ili iwe na ubora unaotakiwa.
Pia, Dk. Mahenge amewaagiza viongozi wa Wakala wa Barabara (Tanroads) na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo wakandarasi kurekebisha barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua wakati wanajenga.
"Ningeomba sisi viongozi tuwe karibu na makandarasi walio site, na bahati nzuri kwa kweli, barabara nyingi zina wakandarasi sasa, wametengeneza halafu mvua zimenyesha zimeharibu, ni vizuri kabla hawajalipwa wawe wamezitengeneza," amesisitiza RC Mahenge.
Maagizo hayo ameyatoa katika kikao cha pili cha Bodi ya Barabara ya mkoa huo kilichofanyika jijini Dodoma Machi 17, 2021 na kuhudhuriwa na viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wenyeviti wa halmashauri, makatibu tawala wa wilaya, wabunge pamoja na baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Pia, katika kikao hicho kinachojadili na kushauri kuhusu hali ya barabara katika mkoa huo, kimehudhuriwa na viongozi wa Jiji la Dodoma, akiwemo Meya wa Jiji, Prof. Davis Mwamfupe, Mkurugenzi wa Jiji, Joseph Mafuru pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na Mjumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa huo, Ismail Jama.
Aidha, katika kikao hicho wajumbe walisomewa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara za Tanroads hadi kufikia Februari 2021, Mpango na bajeti ya barabara za Tanroads kwa mwaka 2021/2022,taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara za Tarura hadi kufikia Februari 2021, Mpango na Bajeti ya Barabara za Tarura kwa mwaka 2021/2022.
Vilevile, wajumbe wamesomewa Mpango wa miradi, mradi wa miji ya kimkakati katika halmashauri ya Jiji la Dodoma hadi Februari 2021, Mpango wa bajeti ya miji ya kimkakati kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka 2021/2022.
Mdau, ni mambo mengi yamejadiliwa kwenye kikao hicho, hivyo nakuomba uendelee kusiliza kupitia clip hii ya video RC Mahenge akitoa maagizo, Katibu Tawala Msaidizi wa Miundombinu Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula akisoma maazimio ya kikao hicho...
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇