LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 4, 2021

RC KUNENGE APOKEA KONTENA 65 NA GARI 20 KWA AJILI YA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge akiwa katika gari moja kati ya 20 baada ya kuzipokea pamoja na konte 65 kwa ajili ya kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, leo

Mkuu wa mkoa Kunenge amepokea  gari na Kontena hizo kwenye Bandari ya Dar es Salaam, na kuyagawa kwa Halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam ambapo Halmashauri ya Jiji hilo akiigawia gari 5, Manispaa ya Temeke gari 8, Kinondoni gari 5 huku Ubungo na Kigamboni wakipewa gari moja moja.


RC Kunenge amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa zote kuhakikisha suala la usafi linapewa kipaombele huku akitaka magari hayo kutunzwa ili yadumu Muda mrefu na kutatua kero ya usafi.


Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuepuka tabia ya kutupa taka kwenye mitaro na mito kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha mitaro kuziba huku akisema watakaohusika kuchafua mazingira Sheria itafuata mkondo.


Kwa upande wake Mratibu wa Miradi ya Bank ya Dunia chini ya TARURA na DMDP Humphrey Kanyenye amesema lengo la miradi wanayosimamia ni kuhakikisha wanaboresha mazingira ya Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira kuwa Safi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages