Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza, baada ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango kuapishwa leo Ikulu jijini Dodoma.
Ikulu, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wabunge watatu na kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo amewabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri na ameteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya.
Akizungumza baada ya Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango kuapishwa, Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Rais Samia aliwataja Wabunge watatu aliowateua kuwa ni;
1. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
2. Balozi Liberata Mulamula na
3. Mbarouk Nassor Mbarouk
Rais Samia alitangaza kumteua Balozi Hussein Athuman Katanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.
Kwa upande wa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Samia aliyataja mabadiliko hayo ifuatavyo;
Ofisi ya Rais.
1.Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
• Waziri – Ummy Ali Mwalimu ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
• Naibu Mawaziri – Dk. Festo John Dugange
• Naibu Waziri - David Silinde
2. Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
• Waziri–Mohammed Omar Mchengerwa
• Naibu Mawaziri– Deogratius Ndejembi
Ofisi ya Makamu wa Rais.
3. Muungano na Mazingira
• Waziri – Selemani Jafo ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa TAMISEMI.
• Naibu Waziri – Hamad Hassan Chande
Ofisi ya Waziri Mkuu.
4. Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
• Waziri – Jenister Joakim Mhagama
• Naibu Mawaziri – Patrobas Katambi
• Naibu Waziri - Ummy Nderiananga
5. Uwekezaji
• Waziri – Geofrey Mwambe ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
• Naibu Waziri – William Tate Ole Nasha
Wizara
6. Wizara ya Fedha na Mipango
• Waziri – Mwigulu Lameck Nchemba ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
• Naibu Waziri– Hamad Yussuf Masauni
7. Wizara ya Katiba na Sheria.
• Waziri – Prof. Palamagamba Aidan Kabudi ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
• Naibu Waziri – Geofrey Mizengo Pinda
8. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
• Waziri – Elias Kwandikwa
9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
• Waziri – Balozi Liberrata Mulamula
• Naibu Waziri – Mbarouk Nassor Mbarouk
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
• Waziri – George Simbachawene
• Naibu Waziri - Khamis Hamza
11. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
• Waziri – Leonard Chamriho
• Naibu Waziri – Geofrey Kasekenya
• Naibu Waziri - Mwita Mwikwabe Waitara
12. Wizara ya Viwanda na Biashara.
• Waziri – Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Uwekezaji.
• Naibu Waziri – Exaud Kigahe
13. Wizara ya Madini.
• Waziri – Dotto Mashaka Biteko
• Naibu Waziri – Shukrani Manya
14. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
• Waziri – William Lukuvi
• Naibu Waziri – Dk. Angelina Mabula
15. Wizara ya Maji
• Waziri – Jumaa Hamidu Aweso
• Naibu Waziri – Mary Prisca Mahundi
16. Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
• Waziri – Innocent Bashungwa
• Naibu Waziri – Pauline Gekul ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi
17. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
• Waziri – Prof. Joyce Ndalichako
• Naibu Waziri – Omar Kipanga
18. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
• Waziri – Dorothy Gwajima
• Naibu Waziri – Godwin Mollel
• Naibu Waziri – Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Waziri wa Fedha
19. Wizara ya Nishati
• Waziri – Dk. Medard Matogolo Kalemani
• Naibu Waziri – Stephen Byabato
20. Wizara ya Maliasili na Utalii.
• Waziri – Dk. Damas Ndumbaro
• Naibu Waziri – Mary Francis Masanja
21. Wizara ya Kilimo.
• Waziri – Prof. Adolf Mkenda
• Naibu Waziri – Hussein Mohammed Bashe
22. Wizara wa Mifugo na Uvuvi.
• Waziri – Mashimba Mashaka Ndaki
• Naibu Waziri – Abdallah Khamis Ulega ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
23. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
• Waziri – Dkt. Faustine Ndugulile
• Naibu Waziri - Kundo Mathew
Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na waliobadilishiwa wizara wataapishwa kesho saa 9:00 Alasiri Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Aidha, Rais Samia ametoa miezi mitatu kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Naibu Waziri wake kuanzisha Wizara hiyo vinginevyo watahesabiwa kuwa wameshindwa kufanya majukumu yao.
Rais Samia amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri hao kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwamba watakaoshindwa kutimiza wajibu wao hatosita kufanya mabadiliko.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇