LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 12, 2021

PAPA FRANCISCO ALISHAWISHIKA NA NINI KIIMANI KUFANYA ZIARA IRAQ, LICHA YA CHANGAMOTO ZA KIUSALAMA NA CORONA KUTANDA NCHINI HUMO?


Papa Francisco

Machi 5 hadi 8, 2021, Baba Mtakatifu Papa Francisco alifanya ziara ya kitume nchini Iraq ikiwa ni mwitikio wa mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Barham Salih akishirikiana na Kanisa Katoliki la nchini humo, ziara hiyo ikiwa ya kwanza rasmi nchini Iraq na safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu kuzuka kwa la corona.


"Ninafikiria kila mara juu ya Iraq, ambapo nataka kwenda mwaka ujao," Papa Francisco alikaririwa akisema katika Mkutano wa Mashirika ya Misaada kwa Makanisa ya Mashariki (ROACO) wakati akijiandaa kwa ziara hiyo ambayo kiongozi huyo alipangiwa kutembelea Baghdad, Mosul na Qaraqosh.


Bila shaka wengi walijiuliza kwa nini Papa Fransisco alilazimika kufanya ziara hiyo nchini Iraq,  akijua fika kwamba katika nchini hiyo kuna changamoto nyingi za kiusalama na Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO- 19) au COVID 29  kupamba moto? Bila shaka wengi hawakupata jibu au majibu ya moja kwa moja juu ya swali hilo.


Hapana shaka, inawezekana zilikuwepo sababu kadhaa zilizomfanya kiongozi huyo wa ngazi ya juu kabisa wa Kanisa Katoliki Duniani, kuamua kuitikia mwaliko wa Rais wa Iraq Barham Salih na kufanya ziara hiyo akiachana na hofu ya kukumbwa na  changamoto nilizotaja hapo.


Hivyo, wakati unayesoma andiko hili unaendelea kujifikirisha sababu hasa iliyomfanya Papa Francisco kufanya ziara hiyo, nadhani siyo vibaya tukadadisi kidogo kwamba pengine historia iliyomo katika Maandiko ndani ya Biblia na vitabu vingine vinavyorandana na kitabu hicho, ndiyo itakuwa sababu kuu iliyomsukuma na kumuongezea hamu kubwa ya kufanya ziara hiyo. Historia yenyewe kwa ufupi na kwa muhjibu wa Biblia ni hii ifuatayo;-


1. Bustani ya Edeni ilikuwa nchini Iraq.

2. Mesopotamia ambayo sasa ni Iraq ilikuwa uoto                          wa ustaarabu!

3. Nuhu alijenga safina nchini Iraq.

4. Mnara wa Babeli ulikuwa nchini Iraq.

5. Abraham alitoka Uru, ambayo iko Kusini mwa Iraq.

6. Rebeka mke wa Isaka anatoka Nahori ambayo iko nchini          Iraq.

7. Jacob alikutana na Rachel nchini Iraq.

8. Yona alihubiri Ninawi ambayo iko Iraq.

9. Ashuru ambayo iko Iraq ilishinda makabila 10 ya Israeli.

10. Amosi alilia akiwa nchini Iraq.

11. Babeli ambayo iko nchini Iraq iliharibu Yerusalemu.

12. Daniel alikuwa kwenye shimo la simba nchini Iraq.

13. Watoto wa Kiebrania watatu walikuwa kwenye moto nchini        Iraq.

14. Belshaza, Mfalme wa Babeli aliona maandishi juu ya                ukuta nchini Iraq.

15. Nebukadreza, Mfalme wa Babeli, aliwachukua                          Wayahudi mateka hadi nchini Iraq.

16. Ezekieli alihubiri nchini Iraq.

17. Watu werevu wengi walikuwa kutoka nchini Iraq.

18. Petro alihubiri nchini Iraq.

19. Dola ya Mtu iliyoelezewa katika Ufunuo inaitwa Babeli              ambayo ilikuwa mji nchini Iraq.


Pia kulingana na Biblia na Vitabu vingine vitakatifu, inafahamika hakuna taifa lingine, isipokuwa Israeli, ambalo lina historia zaidi na unabii unaohusishwa nayo kuliko Iraq.


Ikumbukwe tu kwamba Iraq sio jina ambalo linatumiwa katika Biblia.  Majina ya Iraq yanayotumika katika Biblia ni Babeli, Wakaldayo, Ardhi ya Shinari, na Mesopotamia.  Neno Mesopotamia linamaanisha kati ya mito miwili, haswa kati ya Mito ya Tigris na Frati.  Jina Iraq, linamaanisha nchi yenye mizizi ya kina na kulingana na Biblia ni dhahiri  Iraq ni nchi yenye mizizi ya kina na ni nchi muhimu sana katika Biblia na hizi ndio sababu;-

👉 Bustani ya Edeni ilikuwa Iraq - Mwanzo 2: 10-14

👉 Adamu na Hawa waliumbwa Iraq - Mwanzo 2: 7-8

 đź‘‰Shetani alijitokeza mara ya kwanza katika Iraq- Mwanzo          3:1-6

 đź‘‰Nimrod alianzisha Babeli na Mnara wa Babeli ulijengwa            Iraq - Mwanzo 10: 8-97;  11: 1-4

 đź‘‰Kuchanganya kwa lugha kulifanyika Iraq-Mwanzo 11: 5-11

 đź‘‰Abrahamu alitoka mji katika Iraq - Mwanzo 11:31;                      Matendo 7: 2-4

 đź‘‰Bibi harusi wa Isaka alitoka Iraq - Mwanzo 24: 3-4;  10

 đź‘‰Yakobo alitumia miaka 20  Iraq - Mwanzo 27: 42-45;  31:38

 đź‘‰Dola ya kwanza ya Ulimwengu ilikuwa Iraq-Danieli 1: 1-2;        2: 36-38

👉 Uamsho mkubwa zaidi katika historia ulikuwa katika mji            huko Iraq - Yona 3

👉 Matukio ya kitabu cha Esta yalifanyika Iraq - Esta

👉 Kitabu cha Nahumu kilikuwa unabii dhidi ya mji huko Iraq-        Nahumu

👉 Kitabu au Ufunuo una unabii dhidi ya Babeli ambalo                  lilikuwa jina la zamani kwa taifa la Iraq - Ufunuo 17 & 18


Andiko hili nimelitayarisha kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo Biblia tu kwa kuwa ndicho kitabu chenye Uhusiano wa karibu na Kiongozi niliyemzungumzia hapo Baba Mtakatifu Papa Francisco na lengo kubwa ni kubadilishana uelewa na wewe kuhusu ziara hiyo ya Papa Francisco nchini Iraq. Unaweza kutoa maoni yako kupitia Ukurasa huu au nipigie 0789498008.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages