LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 22, 2021

NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI YAMLILIA HAYATI RAIS MAGUFULI

 


Bendi maarufu ya muziki wa dansi The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, wamepokea kwa masikitiko na uchungu mkubwa msiba wa kifo cha Rais John Pombe Magufuli.Kiongozi wa bendi hiyo mwanamziki Ebrahim makunja aka Kamanda Ras Makunja kwa niyaba ya bendi yake anatoa pole kwa kwa Rais mpya Mama Samia Suluhu Hassan,pole kwa mama Janet Magufuli na familia yake na pole kwa watanzania wote. Bendi ya Ngoma Africa band inaungana na watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kiongozi wetu Rais Magufuli ambaye alikuwa kipenzi chetu na rais aliyejitoa muanga kwa ajili ya wanyonge. Ngoma Africa Band inaungana na watanzania katika maombolezo ya msiba huu.
Mungu ampumzishe Peponi Kiongozi wetu Hayati Rais John Pombe Magufuli – Ameen
MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages