LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 31, 2021

MUTAFUNGWA APIGILIA MSUMARI WA MOTO KWA MADEREVA WA MABASI

 

  KAMANDA Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa madereva wanatakiwa kujiepusha na ajali ambazo kuepukana huko kunatokana na kufuata sheria za usalama Barabarani.


Mutafungwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na madereva kituo cha Mabasi cha Magufuli Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam amesema kuwa madereva hawahitaji mashindano kwani wakitoka kituoni hapo wanakuwa wanapofika katika vituo wanakuta Abiria walishakata tiketi.

Amesema kuwa ajali zinagharimi uchumi wa nchi kutokana na watu hao ni nguvu kazi ya taifa lakini pia wanawategemezi wao.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa dereva wakati wa kusafiri anakuwa na posho hivyo anatakiwa posho yake ale na familia yake ikitokea anavunja sheria posho yake hiyo itakwenda serikalini kwani hakuna mmiliki anayeweza kulipa Makosa ya dereva mzembe.

Aidha amesema kuwa katika kipindi cha sikukuu ya pasaka madereva wanakumbushwa kuendelea kuzingatia sheria za usalama Barabarani ili wananchi washerekee siku kuu bila majozi.

Amesema madereva watakwenda tofauti na sheria watapigwa faini zitawahusu.

Mutafungwa amesema kuwa abiria wanatakiwa kuwa na uhakika na safari zao na sio kuwa na mashaka na madereva kwa wale wenye kazi ya kudhibiti tutashughulika nao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages