Mwenyekiti wa Kijiji cha Manyemba, akifungua kikao cha mafunzo hayo.
Afisa Ushirika wa Wilaya ya Chamwino, Kobelo Isaack akiendesha mafunzo kuhusu umuhimu wa kuanzisha vyama vya ushirika.
Katibu wa Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko cha Ichimada, Stephen Mwalimu akihamasisha wakulima kujiunga na ushirika huo kwa kuwaelezea faida watakazopata.
Wananchi wakihamasika na mafunzo hayo
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Chamwino, Living Kilawe akiwaeleza jinsi ya kufuata kanuni za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
Wakulima wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo
Mmoja wa wakulima akiuliza swali
Mthamini Mwandamizi Wilaya ya Chamwino, Christopher Sanga akielezea umuhimu wa kuthaminisha mali.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chamwino, Fredy Kipanyula akielezea jinsi ya kuchangamkia fursa mbalimbali.
Kijana Mkulima wa Manyemba, akitafakari jambo wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mahusiano na Mikopo wa Benki ya NMB Tawi la Chamwino, Emil Mrumah akielezea umuhimu wa wakulima kujiunga na benki hiyo na faida lukuki watakazopata kutokana na mikopo wanayotoa yenye riba nafuu.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Manyemba, akiwaonesha jinsi ya kujaza kwenye dodoso za hojaji
Lilian Malambo Afisa Ardhi Wilaya ya Chamwino, akiwaelezea wananchi kuhusu hati miliki za ardhi wanazotakiwa kugawiwa Machi 16, 2021.
Diwani wa Kata ya Dabalo, Chamwino, Isihaka Msungilwa akizungumza kwa kutoa shukrani kwa Mkurabita kufanikisha mafunzo hayo yatakayo wanufaisha wananchi wa Manyemba na kata hiyo kwa ujumla.
Na Richard Mwaikenda, Chamwino
MPANGO wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), umewapiga msasa wa mafunzo Wakulima wa Kijiji cha Manyemba, Kata ya Dabalo, wilayani Chamwino, Dodoma, kuhusu mambo muhimu wanayotakiwa kuzingatia kabla ya kuanza kilimo cha mkataba cha miwa na alizeti.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yaliongozwa na Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Antony Temu pamoja na wataalamu wa kilimo, ushirika, ardhi, uthamini wa mali, maendeleo ya jamii na maafisa kutoka Benki ya Nmb.
Wakulima walifundishwa jinsi ya utunzaji wa kumbukumbu mahesabu ya kilimo, kuandaa mpango wa biashara, utafutaji wa fursa, kilimo bora cha miwa na alizeti na jinsi ya kuthaminisha mali.
Meneja huyo wa Mkurabita, amewaasa wakulima hao ambao ardhi yao imesharasimishwa kwa msaada wa Mkurabita, kuzitumia hati za mashamba yao kukopea benki ili wapate fedha sa kusaidia kugharamia kilimo kilimo cha kisasa chenye tija pamoja na kuanzishia biashara zingine.
Amewataka kuzingatia mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yaliyotolewa na wataalam ili yawasaidie kuboresha kilimo na biashara na hatimaye kuwainua kiuchumi.
Afisa Kilimo Wilaya ya Chamwino, Living Kilawe aliwafundisha wakulima kufuata kanuni bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ambazo ni; kuandaa shamba viziri, kupanda mapema, kupanda mbegu bora, kupanda kwa mstari. weka mbolea sahihi ya kupandia na kukuzia, kufanya parizi mapemba na kudhiti wadudu waharibifu.
Pamoja na mambo mengine, Afisa Ushirika Wilaya ya Chamwino, Kobelo Isaack, amewafunisha jinsi ya kuanzisha chama cha ushirika, aina ya ushirika. Manufaa ya kuwa na Chama cha Ushirika ambayo ni; Kuwawzesha wakulima kuwa na mahali pa kukusanyia mazao yao wakati wakisubiri bei nzuri ya uhakika, kutoa fursa inayomwezesha mwananchi kushiriki katika uchumi wa jamii anamoishi.
Mdau, nakuoma uendelee kusikiliza kupitia kwenye clip hii ya video Meneja wa Mkurabita, Anthony Temu akielezea umuhimu wa hati miliki, Afisa Kilimo Kilawe akielezea kanuni za kilimo, Afisa Ushirika, Kobelo Isaack akielezea umuhimu wa kujiunga na chama cha ushirika, Afisa Mwandamizi wa uthamini Christopher Sanga akielezea jinsi ya kuthaminisha mali pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii, Fredy Kipanyula wakitoa mafunzo kwa wakulma hao...
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇