LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 19, 2021

MAMA SAMIA AAPISHWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
Aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia ameapishwa kuwa Rais kuchukua nafasi iliyoachwa wazi kufuatia aliyekuwa Rais Dk. Magufuli kufariki Dunia juzi.

Aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia ameapishwa kuwa Rais kuchukua nafasi iliyoachwa wazi kufuatia aliyekuwa Rais Dk. Magufuli kufariki Dunia juzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupewa Heshima ya kupigiwa Wimbo wa Taifa pamoja na kukagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati akipigiwa Wimbo wa Taifa na Mizinga 21 mara baada ya kuapishwa kuwa Rais. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mama Samia Suluhu Hassan  akitafakari jambo baada ya kuapishwa kuwa Rais

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa kupitia vyombo vya Habari baada ya kuapa Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2021 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan akiongoza kuomba dua alipokwenda kumpa pole Mama Janeth Magufuli baada ya kuapa Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2021 Pamoja naye ni Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Bashiru Ally na Binti wa Marehemu Rais Dk John Pombe Magufuli 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri leo tarehe 19 Machi 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kuwa Rais. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages