LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 12, 2021

MAKUMI WAPOTEZA MAISHA KWENYE MKASA WA MOTO KIWANDANI MISRI


  • Makumi wapoteza maisha kwenye mkasa wa moto kiwandani MisriMakumi ya watu wamefariki dunia huku wengine wengi wakijeruhiwa kutokana na ajali ya moto iliyokikumba kiwanda kimoja cha nguo katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Misri imesema, mkasa huo ulitokea jana Alkhamisi katika kiwanda cha nguo kilichoko katika wilaya ya Obour, viungani mwa mji mkuu Cairo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mbali na watu 20 kupoteza maisha katika ajali hiyo ya jana, wengine zaidi ya 24 wamejeruhiwa na wanatibiwa katika hospitali na zahanati za eneo hilo.

Wazima moto wakiwa kazini

Serikali ya Cairo bila kutoa maelezo zaidi imesema timu ya wataalamu imeanzisha uchunguzi wa kubaini kiini cha moto huo na athari zake katika majengo yanayopakana na kiwanda hicho kilichoko katika jengo lenye orofa nne.

Duru za hospitali zinaarifu kuwa, yumkini idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na majereha mabaya waliyoyapata manusura wa mkasa huo wa jana Alkhamisi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages