Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Dar es Salaam, Tanzania
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ataapishwa leo, Ijumaa, Machi 19, 2021 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla ya uapisho itafanyika Ikulu, Dar es Salaam, saa 4 asubuhi na hivyo Mama Samia atakuwa Rais wa sita wa Tanzania.
Mama Samia ataapishwa kuwa Rais Wa Tanzania kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Rais Dk.John Magufuli kufuatia kufariki Dunia jana jioni.
Hatua hiyo, imekuja kufuatia maekekezo ya Katiba ya Tanzania ambayo kwa mujibu wa Ibara ya 37 (5) ya katiba hiyo ni kwamba endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kuktekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.
Hali kadhalika kwa maelekezo ya Katiba hiyo, baada ya Mama Samia kuapishwa kuwa Rais, atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia 50 ya Wabunge wote.
Kwa mujibu wa Katiba hiyo, kabla ya kuteua jina la atakayekuwa Makamu wa Rais, Mama Samia baada ya kuapishwa, atashauriana kwanza na chama cha siasa anachotoka ambacho ni Chama Cha Mapinduzi (CCM).
saf sana tufanye uapisho then tuendelee na taratbu za kwenda kumzika kipenzi chetu. Tuweni pole Tz na kuwa wavumilivu ktk kpnd hiki.
ReplyDeleteni jambo jema sana kupata mrithi wa kiti cha uraisi na baadae tushirikiane ktk harakat za mazishi ya kipenzi chetu JPM
ReplyDelete