LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 15, 2021

JKT MAFINGA YAPANIA KUZALISHA ZAIDI KWENYE KILIMO, UFUGAJI

 Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 841 KJ, Mafinga, mkoani Iringa, Luteni Kanali Issa Chalamila,akizungumza na waandishi wa habari leo March 14,2021 kabla ya kuanza ziara ya utekelezaji wa miradi ya JKT, ambapo Kikosi hicho ni mahsusi katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na wakuzalisha mitamba pamoja na mbuzi na kondoo.

 

Ng’ombe wa maziwa wanaofungwa katika Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 841 KJ, Mafinga, mkoani Iringa.


Na Happiness Mtweve, Mafinga

KATIKA kutekeleza agizo la Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dk.John Magufuli ya kuyataka majeshi kuyataka majeshi nchini kujitosheleza kwa uzalishaji na kuwa na chakula cha kutosha na ziada kikosi cha Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 841KJ Mafinga kimejikita katika shughuli za Kilimo na Ufugaji ambapo imelima ekari 500 za Mahindi, Maharage na Alzeti.

Pia kimejidhatiti kuboresha shughuli za ufugaji kwa kuongeza Ng'ombe 100 wa maziwa ili waweze kukamua lita 1,000 za maziwa kila siku ambapo kwa sasa wana Ng'ombe 29 wanaokamuliwa kati ya Ng'ombe 120 walionao.

Kaimu Mkuu wa Kikosi Luteni Kanali Issa Chalamila  ametoa taarifa hiyo Mkoani Iringa Wilayani Mufindi, kambi ya JKT 841Kj alipokuwa kizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara maalum ya kutembelea na kukagua miradi ya kimkakati ya kilimo na ufugaji katika vikosi vya jeshi.

Amesema, wao wanatekeleza maagizo ya Mkuu wa Jeshi wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge  ya kuvitaka vikosi vyote vya jeshi kujikita katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kuwa na uhakika wa chakula na ziada ya nchi na kuuza nje ya nchi.

"Huu ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Jeshi la JKT Meja Generali Charles M


buge la kutaka tujitegemee katika kujilisha bila kuitegemea hata Senti moja kutoka serikali, azizo hilo linatokana na agizo la Amiri jeshi mkuu na Rais Dk.Magufuli alilolitoa hivi karibu,....

"Rais aliagiza majeshi tujikite zaidi katika masuala ya uzalishaji kupitia Kilimo na Ufugaji ili yaweze kujitegemea katika masuala mbalimbali bila kutegemea Fedha kutoka Serikali Kuu,"amesema 

Amesema licha ya kwamba kikosi chao kilianzishwa mahususi kwa ajili ya ufugaji lakini hivi Sasa wanafanya na shughuli za kilimo mbapo wamelima hizo ekari 500.

Pia amefanua kuwa miongoni mwa mikakati iliyowekwa na kambi hiyo ni kuanzisha kilimo cha zao Parachichi kuongeza eneo la kilimo kutoka ekari 200 hadi 500 na kuongeza uzalishaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Kuhusu mifugo amesema kwa sasa wana zaidi ya Ng'ombe 120 ambapo kati ya hao Ng'ombe 29 wanaokamuliwa kila siku na wanatoa takribani lita 200 hadi 250.

"Lengo letu ni kuboresha shughuli za ufugaji ili waweze kuzalisha maziwa mengi watakayoweza kuwalisha wananchi wa Mafinga na nje ya mafinga ambapo wanatarajia kuongeza Ng'ombe 100 ambao watakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 1000 za maziwa kila siku,"amesema

Amebainisha kuwa kwa  upande wa mbuzi kwa Sasa wanao mbuzi 192 na mpaka Juni mwaka huu watakuwa wamefikisha mbuzi 300.

Luteni Chalamila amesema hivi Wana zaidi ya Ng'ombe wa kienyeji wapatao 280.

Naye Luteni Francis Breck ambaye ni Mtaalam wa Mifugo katika kambi hiyo amesema kituo kina Ng'ombe wa aiina ya mbili ambao ni Asher na Fishen na wana ekari 22 za malisho ya Mifugo hiyo ambazo wanazitumia zaidi kipindi ha kiangazi.

Amesema ili kuwa na malisho ya uhakika wanatarajia kuongeza ekari 50 za malisho ya majani ya kupanda.

"Umahiri wa mafunzo yenye weredi yanayotolewa katika Kikosi hicho, vijana wanaopitia mafunzo  katika kambi hiyo wanakuwa mabalozi wazuri wenye uzalendo,wachapa kazi pindi wanaporudi uraiani,"amesema.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages