Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (Pichani) atafanya kikao chake na Baraza la Mawaziri, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo saa nne asubuhi.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma, Ikulu, Gerson Msigwa imesema, baada ya kuapishwa atalihutubia Taifa kupitia vyombo vya habari, kabla ya kufanya kikao hicho na Baraza la Mawaziri.
Samia anaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua nafasi iliyobaki wazi kufuatia aliyekuwa Rais Dk. John Magufuli kufariki Dunia juzi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇