LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 15, 2021

ZIARA YA BARAZA LA WADHAMINI WA CCM KATIKA CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU NYERERE, KIBAHA, MKOA WA PWANI JUZI.

Mratibu wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) Emmanuela Kaganda (aliyesimama) akitoa maenelezo kwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah (Wapili kushoto) na ujumbe wake walipotembelea chuo hicho, Kibaha mkoa wa Pwani, juzi. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza hilo la wadhamini Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Pandu Omer Kificho 

Katibu wa Sekretalieti ya Baraza la Wadhamini wa CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Bara Rodrick Mpogolo akizungumza wakati wa kikao cha Baraza hilo na uongozi wa Chuo hicho.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah akizungumza wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea chuo ha Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) , Kibaha mkoa wa Pwani, juzi.  Kulia ni   Mratibu wa Chuo hicho, Emmanuela Kaganda akimsikiliza kwa makini. 
Mratibu wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) Emmanuela Kaganda akitoa maenelezo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa CCM Anna Abdallah na Ujumbe wake, wakati akiwaonesha eneo ambalo litatumika kwa micheZO na Burudani kwenye Chuo hicho. Waliosimama nyuma ni Wajumbe wa Baraza hilo, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Pandu Omer Kificho, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kepteni Mstaafu John Chiligati,  Charles Singili, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay, Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Bara Rodrick Mpogolo ambaye ndiye  Katibu wa Sekretalieti ya Baraza hilo la Wadhamini wa CCM, Katibu wa NEC - Uchumi na Fedha Zanzibar  Afadhali Afadhali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mwalimu Raymond Mwangwala ambaye pia ni Mjumbe wa NEC.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mama Anna Abdallah akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo na Uongozi wa Chuo, mwishoni mwa ziara hiyo. (Picha kwa Hisani ya Mratibu wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Emmanuela Kaganda).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages