LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 10, 2021

WAZIRI WA ZAMANI ARCADO NTAGAZWA AFARIKI DUNIA, LEO



Alcado Ntagazwa

Dar es Salaam. 

Waziri wa zamani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema, Arcado Ntagazwa amefariki dunia leo Jumatano Februari 10, 2021 katika hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu.


Taarifa za kifo cha Ntagazwa ambaye pia ni alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamiii saa 4 asubuhi na baadaye Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika alipoulizwa  alisema ni za kweli.


 â€śNi kweli amefariki, chama kitatoa taarifa baadaye kidogo,” amesema Mnyika.


Ntagazwa alihamia Chadema mwaka 2010 akitoka CCM ambako kwa nyakati tofauti aliwahi kuwa mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages