LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2021

WANAUME WATAKIWA KUVUNJA UKIMYA

 


 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Ddodoma kuhusu hali ya vitendo vya kikatili vinavyoendelea kushamiri katika jamii kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Shilungu Ndaki na kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu Amina Mafita.

************************************

Na Mwandihsi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wanaume kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu ukatili wanaofanyiwa ili kutokomeza matukio ya ukatili nchini.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipotoa tamko kuhusu Vitendo vya Ukatili katika jamii mbele ya waandishi wa habari.

Gwajima amesema vitendo vya ukatili vimezidi kuongezeka hapa nchini akitolea mifano mbalimbali iliyotokea hivi karibuni ya waanfamilia kufanyiana vitendo vya kikatili.

Amesema ukatili haufanywi kwa wanawake na watoto tu lakini hata kwa makundi mengine ikiwemo wanaume lakini wengi wao wamekuwa wakinakaa kimya.

“Wanaume msione aibu, muache kukaa kimya dhidi ya vitendo vya ukatili mnavyofanyiwa. Toeni taarifa mapema kwa mamlaka husika muweze kupata msaada ili kuzuia madhara zaidi kutokea” amesema Gwajima.

Amezitaja sababu za ukatili huu ni pamoja na migogoro ya kifamilia ikiwemo kugombea mali, matatizo ya kisaikolojia na jamii kutotekeleza wajibu wake wa kutunza na kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya familia.

Dkt Gwajima amesema Wizara itaendelea kuchukua jitihada zote kuhakikisha ukatili unatokomezwa kwa makundi yote, lakini jamii pia ina jukumu la kuwalinda makundi yote.

Aidha, amesema Wizara itaendelea kushughulikia mauaji ya wazee na kuwa haitorudi nyuma kupambana na ukatili wa aina yoyote ili nchi na mipaka yake ibaki salama kwa amani, upendo na kujiletea maendeleo.

Naye Afisa Ustawi Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Amina Mafita amesema Wizara imejikita zaidi katika kuelimisha jamii kwa kuunda mabaraza kuanzia ngazi za vijiji na mitaa kwa lengo la kulinda makundi yote.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages