LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2021

WAITARA AIAGIZA NEMC KUSHUGHULIKIA KUONGEZEKA KINA CHA MAJI KATIKA ZIWA MASOGWENDA NA MULYA NA KUSABABISHA MAFURIKO, SINGIDA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mwita Waitara,


Na CCM Blog, Singida

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mwita Waitara, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini na kutoa suluhisho la kuongezeka kwa kina cha maji katika Ziwa Masogweda na Mulya katika Manispaa ya Singida ambayo yamefurika na kuleta madhara katika makazi na mashamba.


Waitara alitoa agizo hilo jana wakati wa ziara ya kikazi mkoani Singida, na kuelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Paskasi Muragiri kuhusiana mafuriko hayo, ambapo pia aliomba zichukuliwe hatua kukabiliana na hali hiyo.


Muragiri alisema ziwa hilo huenda likazingira vijiji hivyo viwili na kusababisha madhara kwa wakazi wanaoishi humo hivyo alitumia nafasi hiyo kumuomba Naibu Naibu Waziri Waitara kulifanyia kazi suala hiyo katika ngazi ya kitaifa.


Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine Waitara alitembelea pia machinjio katika Manispaa hiyo na kuitaka Halmashauri hiyo kuharakisha mpango wa kuhamisha machinjio hayo kwenda eneo lingine walilotenga.


“Niwapongeze viongozi wa Manispaa ya Singida nimesikia hapa mna mpango wa kujenga machinjo nyingine kwani baada ya hii na nina imani itakuwa ya kisasa na itakidhi mahitaji maana sasa hivi ninyi ni Manispaa na mnahitaji eneo kubwa kuliko hili,” alisema.


Waitara alitembelea Soko Kuu la Manisoaa hiyo na kuridhishwa na hali ya miundombinu ya kuhifadhi taka ngumu pamoja na dampo lililopo katika eneo la Manga nje kidogo ya Manispaa hiyo.


Akizungumza katika kikao na Maafisa mazingira kutoka Manispaa hiyo Waitara alisema ipo haja ya kuwashirikisha wananchi katika maeneo yao katika masuala ya kuhifadhi mazingira ili kupata taarifa kutoka kwenye vijiji ngazi ya chini.


Naibu Waziri Waitara yuko katika ziara mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Mazingra ya mwaka 2004 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan upandaji na utunzaji wa miti kwa kila halmashauri.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages