Wajumbe wa Kamati ya Uongozi na baadhi ya watumishi wa Mkurabita wakiwa wamesimama wakati Rais wa Zanzibar, Dkt Mwinyi akiingia kwenye kikao nao.
Makamu Mwenyekiti wa Mkurabita, Immaculata Senje akijitambulish kwa Rais wakati wa kikao hicho Ikulu, Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Mkurabita, akielezea kuhusu utendaji wa Mkurabita Zanzibar ambapo wameahidi kwa miaka mitano watajenga vituo 10 jumuishi vya biashara katika wilaya 10 za Unguja na Pemba.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wakisikiliza kwa makini wakat Rais akizungumza nao.
Baadhi ya wajumbe wa Mkurabita wakiwa katika kikao hicho na Rais wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita pamoja na watumishi wa mpango huo.
wajume wa Mkurabita akiondoka Ikulu baada ya kumaliza kikao na Rais Dkt Mwinyi.
Na Richard Mwaikenda, Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza uongozi wa Mpango wa Urasimishaji wa Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), kwa kazi nzuri ya kusaidia kupunguza umasikini kwa kurasimisha mali na biashara za wanyonge visiwani humo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDARais, Dkt. Mwinyi alizitoa pongezi hizo baada ya kusomewa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Immaculata Senje taarifa ya hatua walizofikia za urasimishaji ardhi na biashara za wanyonge Zanzibar Februari 11, 2021 Ikulu, Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti Senje alisema kuwa baadhi ya waliosajili mali zao wameanza kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia hatimiliki kukopea fedha katika mabenki.
Alitaja baadhi ya benki zilizokubali kukopesha kuwa ni Benki ya Watu wa Zanzibar na Amana Bank ambazo maofisa wao walitoa mafunzo kwa wakaazi wa Shehia ya Welezo, Wilaya ya Magharibi A waliokabidhiwa hati hizo.
Senje alimweleza Rais Dkt Mwinyi kuwa Mkurabita wana mpango ndani ya miaka mitano kujenga vituo 10 jumuishi vya usajili wa biashara katika wilaya 10 za Unguja na Pemba, kusajili wafanyabishara 1500 na kurasimisha viwanja/ardhi 5700 Zanzibar.
Mwanzoni mwa wiki Mkurabita imezindua Kituo Jumuishi cha usajili wa biashara eneo la Darajani Zanzibar ambacho kina ofisi za taasisi mbalimbali ambapo kinasaidia kuwapunguzia wananchi usumbufu kwa kupata huduma muhimu eneo moja.
"Ni sahihi hili huwa nalisemea, tuna migogoro mingi huku Zanzibar sababu kubwa ni watu kutokuwa na hatimiliki.
Mpango huu utatusaidia zaidi kufufua mtaji mfu na kuondoa migogoro ya ardhi, pia vituo jumuishi vitasaidia wahusika hupata huduma eneo moja katika kituo kimoja ndivyo inavyotakiwa," amesema Rais Dkt Mwinyi..
"Nataka niwahakikishie kuwa serikali itawaunga mkono kwani hizo zilikuwa ahadi zetu. tutashirikiana nanyi kuona fedha zinatengwa kwa ajili ya mpango, na bajeti tutakayoitenga itaendana na ukubwa wa kazi hii.
Kazi yenu ni nzuri sana itasaidia sana na inaendana na vipaumbele vyetu vya kuwasaidia wanyonge ya kurasimisha kuondoa ule mtaji mfu,"amesema Rais.
Ndugu nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue zaidi yaliyozungumzwa kwenye kikao hiki cha Rais Dkt. Mwinyi na uongozi wa Mkurabita uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Mkurabita, Senje pamoja na Mratibu wa mpango huo, Dkt. Seraphia Mgembe...
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇