LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 19, 2021

RAIS DK. MAGUFULI AONGOZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KATIBU MKUU KIONGOZI JOHN KIJAZI, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akionekana kujawa majonzi wakati mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi ulipokuwa ukifikishwa kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021 ya Ibada maalum ya kuaga na kutolewa heshima za mwisho. Balozi Kijazi alifariki Dunia juzi saa 3 usiku jijini Dodoma.

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi ukiwa umefikishwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Waombolezaji wakijiandaa kushuka kutoka kwenye gari jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi baada ya kufikishwa kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaamushusha kuto

Rais Dk. John Magufuli akiwa amesimama kuonyesha heshima ya kuupokea mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi ulipowsilishwa kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi likipelekwa katika eneo maalum la mwili kufanyiwa ibada maalum na kuagia.

Padre Dk. Joseph Matumaini akiongoza ibada ya kumuaga Marehemu Balozi Injinia John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es slaam leo Ijumaa Februari 19,2021, baadaye mwili wa Dk. Kijazi ulisafirishwa kwenda Korongwe mkoani Tanga ambako utazikwa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla katika Viwanja vya Kareemjee Jijini Dar es salaam leo wakati wa kuagwa mwili wa Marehemu Mhandisi Balozi John William kijazi. Katikati ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Hemedi Suleiman Abdallah (kulia) ni miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari  19,2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ali na Waziri wa Sheria na Katiba Dk.Mwigulu Nchemba wakiwa katika Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi Injinia John Kijazi.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi (kulia) akiwa pamoja na Ndugu na jamaa wakati wa kuaga mwili wa ndugu yao Marehemu Injinia Balozi John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mhandisi Balozi John William kijazi.

 

Baadhi ya Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali wakipita na kutoa heshima zao za mwisho kwa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi Injinia John Kijazi.

Rais Dk. John Magufuli akiwapa pole na kuwaaga Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, kabla ya kuondoka baada ya kutoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Kijazi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiisalimia na kuifariji familia ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Kijazi, kabla ya kuondoka baada ya kutoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa Marehemu Kijazi, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Baadaye mwili wa Kijazi ulisafirishwa kwenda Kuzikwa Korogwe mkoani Tanga.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages