Rais Dk. John Magufuli akimuapisha Dk. Bashiru Ally kuwa katibu Mkuu Kiongozi, katika hafla iliyofanyika leo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais Dk. John Magufuli, amemuapisha Dk. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi wa Tanzania, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dk. Bashiru aliteuliwa jana jioni, na anachukua nafasi iliyoachwa kufuatia kifo cha aliyekuwa katibu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Kabla uteuzi Dk. Bashir alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, tangu Mei, 2018 alipoteuliwa kushika nafasi hiyo badala ya Abdulrahman Kinana uteuzi huo ulifanywa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na kuthibitishwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama ikiwa ni siku kadhaa tangu msomi huyo aongoze mchakato wa kuhakiki mali za CCM.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Idara ya Sayansi ya siasa na alikuwa akiongoza Kurugenzi ya Mijadala na Makongamano.
Dk. Bashiru Ally sasa anakuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa tisa. Makatibu Wakuu Kiongozi waliotangulia na miaka yaliyoanza kuhudumu ikiwa katika mabano ni Dk. John Kijazi (2016), Ombeni Sefue (01/01/2012), Philemon Luhanjo (01/01/2016), Martern Lumbanga (11/02/1995), Paul Rupia (01/07/1986), Thomas Apiyo (22/06/1974), Dickson Nkombo (28/06/1967) na Joseph Namata (30/07/1964).
Makatibu Wakuu Kiongozi wakiotanguliwa na Dk. Bashiru
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇