LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 25, 2021

PANGENI MIKAKATI THABITI YA MAENDELEO KWA JAMII-DK JINGU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu akizungumza katika kongamano la Watalaam wa Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma leo, kwa kuwataka kupanga mikakati thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Katibu Mkuu Dk. John Jingu akisisitiza jambo


Sehemu ya wataalam wa maendeleo ya jamii wakisikiliza kwa makini Katibu Mkuu, Dk. Jingu akizungumza wakati wa mkutano huo.



 Na Richard Mwaikenda, Dodoma

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu amewapiga msasa wataalam wa maendeleo ya jamii kwa kuwataka kupanga mikakati thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Akizungumza katika kongamano la wataalamu hao Dk. Jingu amesema kuwa uongozi wa kimkakati ni uongozi unaoleta mabadiliko, hivyo ni lazima wafanye kazi kimkakati na kwa mafanikio makubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo.

 "Kazi yenu pia ni kubadilisha fikra za watu na ili uweze kufanya hayo inabidi uwe na sifa  ya kuwa na uwezo wa kujenga timu ya kufanya kazi. Huwezi kufanya kazi peke yako, hilo ni kosa na kisaikolojia ni hatari sana lakini kubwa sana kufanikisha mkakati uwe ni mtu wa kusikiliza," amesema Dk Jingu. 

Dk. Jingu ametaja pia sifa zingine  anazopaswa kuwa nazo kiongozi kuwa ni kusoma hisia za jamii inayomzunguka na kuziheshimu, kuheshimu mila na desturi ya jamii anayoihudumia pamoja na kujua mabadailiko anayowapelekea endapo wanayakubali ama wanayakataa.

Amewataka kuwa waadilifu, wawajibikaji na kutii miiko ya kutopokea rushwa, kutokuwa na upendeleo, ama sivyo watakosa imani katika jamii wanayoihudumia.

"Mnatakiwa kuwa na haiba nzuri inayokubalika katika jamii, walimu wana haiba yao, watumishi wa umma pia wana haiba yao hivyo mdumishe utaratibu huo, mtaheshimika," amesisitiza Dk. Jingu.
 
Dk. Jingu alimazia kwa kuwaasa watalaamu hao wa maendeleo ya jamii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwamba watakuwa huwaitendei haki jamii na taaluma yao, hivyo kuwataka kufanya kazi kimkakati kwa kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.

Kongamano hilo lililofunguliwa juzi na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima  limehudhuriwa na wataalam wa maendeleo ya jamii 400 kutoka mikoa yote nchini. Kesho wanafanya mkutano mkuu ambapia pia watafanya uchaguzi wa viongozi wa kukiongoza chama chao cha Codepata.

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Dk. John Jingu akizungumza  kwenye mkutano huo....

Imeandaliwa na; Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203

1 comment:

  1. Taarifa nzuri lakini Maafisa Maendeleo hawana tabia ya kutembelea vikundi kujua maendeleo ya vikundi wanaendeleaje bali wamekaa ofisini kazi yao nikupiga simu kuulizia malejesho hawafiki hata kuona maendeleo yakovipi

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages