Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Mhandisi Atashasta Nditiye (Pichani) amefariki dunia jijini Dodoma, leo asubuhi.
Taarifa ya Spika Job Ndugai imesema, Nditiye amefariki akiwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupatwa na ajali ya gari lake kugongwa na daladala katika eneo la Kisasa jijini Dodoma, juzi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇